IMG_3224
Msanii mkongwe wa HIP HOP nchini Prof. Jay akitoa burudani kwenye tamasha kubwa la kihistoria la Tigo Music Kiboko yao lililofanyika viwanja vya leaders jana.
IMG_3245
IMG_3024
Msanii JUX akitoa burudani kwenye tamasha kubwa la kihistoria la Tigo Music Kiboko yao lililofanyika viwanja vya leaders jana.
IMG_2986
IMG_2935
Vanessa Mdee akitoa burudani kwenye tamasha kubwa la kihistoria la Tigo Music Kiboko yao lililofanyika viwanja vya leaders jana.
IMG_2939
Tigo Tanzania leo imetangaza rasmi uzinduzi wa Muziki wa Tigo ujulikanao kama “Tigo Music” kwa kushirikiana na Deezer, ambayo ni huduma ya kimataifa inayorusha muziki  itakayowapa Watanzania muziki usiokuwa na kikomo.

Hafla ya uzinduzi kwa ajili ya Tigo Music imefanyika katika viwanja vya Leaders Club Dar es Salaam Tarehe 24 Januari ambapo wananchi wametumbuizwa na nyimbo tofauti tofauti kutoka kwa wasaniii 18 wa hapa nchini kama Diamond Platinum, Ali Kiba, Professor J, Weusi, Msondo, Ben Paul, Shillole Linah, Christian Bella, AY hao ni kati ya 18.

Kuanzia Januari 24, wateja wa Tigo wenye vifurushi vya malipo ya kabla ya intaneti wana uwezo wa kupata nyimbo milioni 36 za wasanii wa Kitanzania na Afrika kwa ujumla katika simu zao za mkononi za smartphone. 

 Vilevile, Tigo itatafuta miziki mipya ya kusisimua ya wasanii wa ndani kupitia ushirikiano mpya na kampuni ya Africa Music Rights, ambayo inawezesha, kutafuta na kusimamia haki za muziki katika bara la Afrika,
Meneja Mkuu wa Tigo Bi, Cecile Tiano alisema, ‘Tuna furaha kuwa kampuni ya kwanza ya mawasiliano Tanzania kuwapa wateja wetu muziki usiokuwa na kikomo”. 

Muziki unajukumu kubwa katika Tanzania yetu tajiri na tamaduni tofauti kama starehe katika matukio ya kijamii na hata wakati binafsi. Haya ni mafanikio makubwa kwetu tukitarajia watu zaidi na zaidi kutumia smartphones katika sehemu hii ya dunia’.

“Kama bidhaa yenye maisha ya kidijitali, lengo letu ni kuiwezesha tasnia ya muziki kwa kujenga jukwaa ambalo si tu linaruhusu kupata nyimbo za wasanii wa ndani kwa urahisi, lakini pia linawapa mafunzo wanamuziki wetu kwenye masuala muhimu kama vile haki miliki na masoko. Hii ni njia yetu ya kusaidia vipaji vya wasanii na kukuza tasnia ya muziki wa ndani, “aliongeza.

Kuanzishwa kwa Muziki wa Tigo (Tigo Music) nchini Tanzania kumetokana na mafanikio ya uzinduzi nchini Amerika ya Kusini mwaka 2012 pamoja na Ghana mwaka 2014, na. Tangu kuanzishwa kwake imekuwa ni sehemu muhimu kwa maisha ya kidijitali ya watu ya kila siku na hii inaendana na matukio ya muziki wa ana kwa ana yaliyowahi kufanywa na wanamuziki mashuhuri duniani, pamoja na yale yaliyorekodiwa ndani ya studio.

Kama bidhaa, Tigo music imeongezeka kwa kiasi kikubwa huko Colombia kama nchi inayoongoza  kwa huduma  ya urushwaji wa muziki, wakiwa na watumiaji 600,000 wakisikiliza kwa wastani nyimbo zaidi ya  400 na masaa 40 ya muziki kila mwezi.

Urushwaji wa muziki ni eneo linalokua kwa haraka sana katika tasnia ya muziki kimataifa, na bidhaa ya muziki tayari imekuwa ya pili kimaarufu kwenye vipengele vya simu za mkononi katika Afrika.