Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Migombani-Segera, Japhet Albert Kembo akiapishwa jana jijini Dar es Salam.
...........
Baada
ya kusubiri kwa muda wa wiki mbili ili wajumbe serikali ya mtaa wa
Migombani-Segerea waapishwe na mamlaka husika bila mafanikio, wananchi
wameamua kuwaapisha viongozi hao kwa kutumia wakili binafsi.
Tukio
hilo limetokea jana asubuhi katika ofisi za Serikali za Mitaa zilizopo
Segerea Mwisho ambalo lilijumuisha kuapishwa kwa Mwenyekiti wa Mtaa,
Japhet Albert Kembo pamoja na wajumbe watatu ambao ni Rose Benard
Mhagama, Nyangeto Flora Justin na Ramadhan Rashid Seif.
Akizungumza
baada ya kuapishwa, mwenyekiti mpya wa mtaa huo amesema kuwa wananchi
wamechoshwa na danadana wanazopigwa na Halmashauri ya Manispaa ya Ilala
za kutowaapisha viongozi waliowachagua ndiyo maana wamefikia hatua hiyo
ili kuwakumbusha kutekeleza majukumu yao kwa wakati.
“Wananchi
wanahitaji huduma kutoka kwa watu wanaowaamini lakini wanakosa imani
pale uongozi wa manispaa unaposhindwa kutekeleza majukumu yake kama
inavyotakiwa kwa mujibu wa sheria. Wamemtafuta wakili ambaye amekuja
kulisimamia suala hili kisheria na ndiyo maana zoezi limefanywa
hadharani,” alisema Kembo.
Wananchi
waliozungumza walisema kuwa hawaelewi kinachoendelea kwakuwa uchaguzi
ulifanyika kama kawaida pasipo dosari yoyote na matokeo yakatangwazwa
huku nafasi zote zikichukuliwa na wagombea kutoka Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (Chadema).
“Uchaguzi
wetu haukuwa na matatizo na ni miongoni mwa mitaa iliyotangaza matokeo
muda mfupi baada ya uchaguzi kufanyika lakini jambo la kushangaza ni
kwamba viongozi wote waliochaguliwa hawajaapishwa kama ilivyofanyika kwa
wengine katika manispaa hii wakati hakuna pingamizi lolote mahakamani
linalozuia uhalali wa waliochaguliwa,” alisema John Kandeo, mmoja wa
wananchi walioshuhudia kuapishwa kwa viongozi hao.
Akifafanua
kuhusu matokeo ya uchaguzi uliofanyika Desemba 14, mwaka jana, Kembo
alisema kuwa walikuwa wagombea watatu katika nafasi ya uenyekiti ambao
ni yeye mwenyewe aliyepata jumla ya kura 547, Uyeka Idd wa CCM aliyepata
kura 273 na Erick Mchata wa NCCR-Mageuzi aliyepata kura 205.
Zoezililivyokuwa
Muda
wa saa 05:00 asubuhi, wakili wa kujitegemea kutoka kampuni ya mawakili
ya Ame and Company, Idd Msawanga aliwasili katika ofisi za mtaa huo na
kupokelewa kwa kelele nyingi za wafuasi wa Chadema waliokuwa wakipaza
sauti zao kwa sauti kubwa za ‘Peoples…Power.’
Wakili
Msawanga alianza kwa kumuapisha mwenyekiti, peke yake, na baadaye
wajumbe hao watatu kwa pamoja na kuelezwa kuwa wajumbe wawili hawakuwepo
kutokana na matatizo ya kifamilia.
“Sheria
ya uchaguzi inaruhusu kufanya hivi na hata hao wajumbe wawili ambao
hawapo kwa leo watakaporudi nitawaapisha…ni suala la kutaarifiana tu,”
alisema Msawanga.
Post a Comment