Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

SIMBA SPORT CLUB YAJA KIDIGITALI ZAIDI

Afisa Mtendaji Mkuu wa  EAG Group Imani Kajula Akimwelezea Jambo Rais wa Simba Sport Club Evans Aveva (Aliyekaa) Wakati wa Uzinduzi wa Tovuti ya Club Hiyo Anayeshuhudia ni Makamu wa Rais wa Club ya Simba Geofrey Nyange ‘Kaburu

Simba Sports Club leo hiiimezindua tovuti yake Ili kukuza  mawasiliano  na  wadau wake mbalimbali  hususani; wanachama, wapenzi, vyombo  vya  habari na wadau wengine muhimu. 

Akizungumza  wakati  wauzinduzi  huo  Rais  wa  Simba Evans Aveva  alisema ‘’Katika dunia na zama  za utandawazi  tovuti  ndio  na  mitandao   ya   jamii   ndio  njia  kuu ya mawasiliano. Sisi  tuliliona  hili  na  leo  hii  nafurahi  kuwa  Simba Sports Club itazindua  rasmi  tovuti  yake  ambayo  itakuwa  jukwaa  kuu la mawasiliano  na utoaji wa taarifa zake za  club ya   Simba. Natarajia wengi wenu mtaitumia kikamilifu na muhimu zaidi mtatupa mrejesho chanya kuhusu  tovuti yetu’’. 

AfisaMtendajiMkuuwa EAG Group Imani Kajula ambao ni washauri watekeleza ji wa Masokona Biashara wa Simba alisema ‘’Tovuti hii sio tuitaiwezesha Simba kuwapa wadau wake taarifa mbalimbalibali pia  itatumika  kwa  ajili  ya uuzaji  wa  vifaa  vya  Simba, Bidhaa  mbalimbali  mpya  na  muhimu  zaidi  kuwaunganisha   wanachama, mashabiki  na wapenzi wa  Simba  kutumia   mitandao  ya  jamii  iliyo   rasmi  ya  Simba Sports Club’’. 

Mkutano   huo  wa  wandishi  wa  habari   ulitumika  kutaarifu   Wanachama, Wapenzina  Vyombo   vya   habari   juu   ya  kocha   mpya   wa   Simba. Alizungumza  wakati  wakumtambulisha   kocha   mpya   wa   Simba, Rais   Aveva   alisema ‘’Baada ya kupitia  vyeti  na  maombi   ya  makocha   mbalimbali, Napenda  kuwa taarifu kuwa Klabu ya Simba imeingia  kwenye  mkataba  wa   kuifundisha   na   kocha Dylan Kerr raia   wa   Uingereza. Ni kocha   mwenye    uzoefu   wa   zaidi   ya   miaka 30, akiwa  amefanya  kazi  Nchi  mbalimbali  zikiwemo    Uingereza, Scotland, Vietnam   na    AfrikayaKusini’’. 

Aliendelea  kusema ‘’Tunaamini   ujuzi   na   uzoefu wake wa  ukocha na pia kama mchezaji wa kiwango cha juu  utakuwa   chachu   ya   kuifanya   Simba    ifanye    vizuri’’
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top