Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa
habari kwenye ukumbi wa Sekretarieti mjini Dodoma.(Picha na Adam Mzee)
…………………………………………………………………………
“Leo tarehe
7 mwezi wa saba tunaanza vikao vya mchakato wa mkutano mkuu wa taifa wa
CCM ambao unnategemewa pamoja na mambo mengine utapitisha ilani ya
uchaguzi ya mwaka 2015-20 20 lakini pia utateua mgombea wa urais
wa jamhuri ya muungano wa tanzania kupitia CCM, na pia kutakuwa na
kikao cha halmashauri kuu ambacho kitateua jina la mgombea wa urais kwa
chama cha mapinduzi kwa upande wa Zanzibar, ratiba ya vikao, leo tarehe
7 kuanzia saa tano tutakuwa na sekretarieti ya halmashauri kuu ya
Taifa ya chama cha mapinduzi ambacho kitaongozwa na Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana.
sekretarieti hiyo ina ajenda moja kubwa kwa kupitia maandalizi ya mkutano mkuu, ina ajenda kubwa ya kupitia maandalizi ya mkutano mkuu na kuthibitisha yapo mambo mengi katika maandalizi kuna mambo ya ratiba, mambo ya malazi ya wajumbe, kuna mambo ya makablasha mbalimbali na maandalizi ya document mbalimbali zitakazotumika kwenye vikao vitakavyoendelea baada ya leo.
Kesho tarehe
8 kunategemewa kufanyika kikao cha kamati ya usalama na maadili cha
chama, ambacho kitakuwa chini ya mwenyekiti wa Taifa Dk.Jakaya Mrisho
Kikwete.
Tarehe
9 kichama kutakuwa na shughuli kuu mbili ya kwanza asubuhi, kutafanyika
uzinduzi au ufunguzi wa ukumbi mpya wa chama cha mapinduzi na ofisi
zake ambao upo njia ya kwenda chuo kikuu cha Dodoma bila shaka baadhi
yenu mtakuwa mmeona, mwenyekiti wa chama Rais Kikwete alipokwenda
kutembelea kwahiyo ufunguzi wake utafanyika tarehe 9, majira ya asubuhi
kabla mheshimiwa rais hajaenda kuvunja bunge, kama ratiba itabadilika
tutawaambia lakini tarehe 9 tunahiyo shughuli ya kwanza baadaye mchana
kutakuwa na kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa ya chama
cha mapinduzi ambayo nayo ni muendelezo wa vikao vya awali kuelekea
mkutano mkuu.
Tarehe 10
tunategemea kuwa na kikao cha Halmashauri kuu ya chama cha
Mapinduzi ambacho kikao hichi kitafanya mambo makubwa matatu ambacho
kitafanya, kwanza kitateuwa jina la mgombea urais kwa upande wa Tanzania
zanzibar, halmashauri kuu ya taifa kwa mujibu wa katiba ndio inayoteua
jina la mgombea urais wa Zanzibar kwahiyo hiyo itakuwa ni kazi
mojawapo itakayofanywa na Halmashauri kuu ya Taifa na kazi ya pili,
watapitia pia ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi ambayo ndiyo
itakayotumika kuombea kura na ndio itakayotumika kwa kipindi cha
2015-2020, na kutoka kwao hiyo ilani itapelekwa katika mkutano mkuu
kwaajili ya kuhitimishwa.
Kazi ya
tatu, halmashauri kuu hii itapokea majina matano kutoka kamati
kuu ambayo yatakuwa yameteuliwa na kamati kuu, tarehe 9 na hapo
watafanya kazi ya kupiga kura kupata majina matatu ya wanachama wa CCM
walioomba kupitishwa na chama cha mapinduzi kuwa wagombea wa nafasi ya
urais kwa upande wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Majina matano
haya yatapigiwa kura kupata matatu na tarehe 11 ndio siku ya mkutano
mkuu wa Taifa wa chama cha mapinduzi ambao una kazi kubwa mbili, moja ni
kupitisha hiyo ilani ambayo itakuwa imepitishwa na halmashauri kuu ya
Taifa na maandalizi ya ilani hiyo yamekamilika, tuliunda timu kama
mnakumbuka tumewahi kuitangaza ipo chini ya Wasira imefanya kazi nzuri
ya kutengeneza ilani nadhani safari hii tutakuwa na ilani nzuri sana
ambayo itaendeleza mafanikio yaliyopatikana katika awamu zote zilizopita
lakini pia itatupeleka sasa kwenye hatua kubwa zaidi ya maendeleo ya
nchi yetu.
Kazi
ya pili, ni kupiga kura katika majina matatu yatakayowasilishwa katika
mkutano mkuu ili kupata jina moja la mwanachama wa CCM ambaye ndiye
atakuwa mgombea wa urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia
chama cha mapinduzi, hivyo tarehe 11, itakuwa ni siku ya mkutano mkuu na
mkutano mkuu huu utakuwa wa siku moja,lakini mkutano mkuu huu
utaoneshwa moja kwa moja kupitia vyombo mbalimbali vya habari hapa
nchini, tv zote zitaonesha kuanzia ufunguzi ratiba ile mpaka wakati
fulani halafu baadaye wakati wa matokeo na ufungaji wa mkutano karibia
masaa sita au saba hivi tutauonesha moja kwa moja.
Ninachotaka
tu ni kuwathibitishia watanzania tumejipanga vizuri chama chetu tupo
wamoja tunaamini tutamaliza vikao hivi salama, na tutatoka tukiwa na
ushindi, tutatoka tukiwa na nguvu, tutatoka tukiwa wamoja na bila shaka
vikao hivi vitajenga msingi wa kushinda uchaguzi kwa kishindo sana mwaka
huu.
Nataka pia
nichukue nafasi hii kuwathibitishia wajumbe wa vikao vyote
kuwa maandalizi yao yamekamilika na tunawatakia safari njema kutoka
wanapotoka katika nchi yetu, tunawatakia afya njema na vikao vyema vya
kamati ya maandalizi na tunawakaribisha sana Dodoma karibuni tukijenge
chama chetu na demokrasia ya nchi yetu tuendelee kuimarisha demokrasia
ya nchi yetu”.
Post a Comment