Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

LOWASSA KUZUNGUMZA NA WANAWAKE LEO


Mgombea urais wa CHADEMA kupitia UKAWA Mh Edward Lowassa leo anatarajia kuzungumza na makundi mbalimbali ya wanawake kabla ya uzinduzi wa kampeni kwa kueleza mipango alionayo katika kuinua uchumi wa wanawake na kupambana na umasikini

Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chama hicho Mh.Halima Mdee akizungumza jijini Dar es Salaam jana amesema Mh Lowassa pamoja na viongozi mbalimbali wa CHADEMA, watazungumza na wawakilishi wa makundi mbalimbali ya wanawake ambapo atazungumza mikakati alionayo kwa wanawake na watoto na hatma ya maendeleo kwa taifa

Aidha Mdee amesema Lowassa atapata fursa ya kuainisha kuhusu watoto wa kike wanaokosa fursa za elimu , sekta ya kilimo ambayo ina ajiri wanawake wengi pamoja na sekta ya afya.

Katika hatua nyingine ya Kampeni Mdee amesema BAWACHA wamegawa kanda kumi kuhakikisha wanawafikia wanawake katika mikoa yote kupeleka ujumbe wa matumaini kwa wanawake kushiriki harakati za ukombozi kwa taifa lao

author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top