Wanaume wa shoka wakilisakata rhumba wakati wa kuwafurahisha mashabiki wa bendi ya Skylight wakati wa mkesha wa eid
Mwimbaji
wa bendi ya Skylght Natasha akiwa anawapa mashabiki vionjo vya nyimbo
za taratibu (kistaarabu) wakati wa mkesha huo wa Eid ndani ya kiwanja
cha Escape One Mikocheni
Bendi
ya waimbaji wakali wa Skylight ikirindimisha baadhi ya nyimbo zao huku
mbele kabisa akiwa anawaongoza wenzake katika uimbaji wa nyimbo hiyo
Sony Samba.
Ashura Kitenge (kushoto) akiwa na Kasongo Junior wa Skylight band wakitoa burudani ya kukata na shoka kwa mashabiki wao ndani ya kiwanja cha Escape One Mikocheni
Sam
Mapenzi ni muimbaji mashuhuri na huwa anajua kukonga nyoyo za watu
hususani katika ule muziki wa Afrika magharibi weee utampenda hata kwa
mkopo, hapo akiwa anaimba kwa kushirikiana na wenzake ndani ya bendi ya
Skylight siku ya mkesha wa Eid.
Baadhi ya waimbaji wa bend ya Skylight wakitoa burudani kwa mashabiki wao usiku wa kuamkia sikukuu ya Eid.
Hii
siku zote huwa inapatikana ndani ya Skylight tu na sio kwingineko maana
ukihitaji kuburudika njoo tuungane pamoja katika bendi yetu inayoenda
kwa kusikiliza mashabiki zaidi na sio kubagua mashabiki.
Ile
kauli ya mteja ni mfalme inadhihirika hapa wakati mashabiki wameamua
kuungana na waimbaji wa bendi yao ya Skylight ili kuhakikisha mambo yote
yanaenda sawa kiburudani zaidi.
Kwa
style tofauti tofauti fika uungane na Skylight band ili uweke shida
pembeni na kuweza kufurahia maisha ni kila siku ya Jumapili tukutane
ndani ya Escape One Mikocheni kukonga nyoyo zetu na Skylight band
Mashabiki sasa zamu yao kulisakata wakati bendi ya Skylight ikiwa inatoa burudani hiyo ndani ya Escape One Mikocheni
Rapa
mkongwe kwenye muziki wa Live Joniko Flower akiwa katika hatua yake ya
kukusanya mashabiki ili tu waende sawa aisee huyu jamaa ni hatari
jumapili hii atakuwepo pale Escape One Mikocheni bila kukosa sogea
taratibu uje ushuhudie vitu kutoka Skylight band.
Sony
Masamba mwenye nguo nyeupe wa kwanza ambaye ni muimbaji wa bendi ya
Skylight akienda sawa na mashabiki wa bendi hiyo kwa kulisakata rumba
mashabiki wa bendi ya Skylight wakiserebuka kwa raha zao wenyewe fika na wewe ili upate burudani ya kukata na shoka.
Kasongo
Junior akitoa burudani ya kuwaimbia mashabiki wa bendi ya Skylight
kwani yeye ni mtaalamu wa sauti yenye mvuto mkubwa ambapo huto tamani
kukosa kumsikiliza kila aingiapo jukwaani.
Sam Mapenzi akiwa katika ishara ya kuimba kwa hisia ndani ya viwanja vya Escape One Mikocheni kwenye mkesha wa Eid
ukafika ule wakati wa shock dance hapo sasa fika jumapili hii ili upate vitu hatari kutoka Skylight band
New
style ya nyimbo yao ni pamoja na hii hapa wakiwa wameweka mkono mmoja
kwa hewa ,Skylight band Wazee wa style mpaka wewe mwenyewe useme basi
Sam
Mapenzi (kushoto) akiwa na Ashura Kitenge wakitoa burudani ya nguvu
ndani ya Skylight band wakati wa mkesha wa kuamkia sikukuu ya Eid
Vijana wa Skylight band hao katika ubora wao fika uone jinsi wanavyo kupeleka katika mapumziko ya fikra zako.
Mmoja wa viongozi wa Bendi ya Skylight Joshua Ndege (katikati) akionyesha umahiri wake sambamba na waimbaji wa bendi hiyo.
Kushoto Rapa
mkongwe katika muziki wa Live Joniko Flower pamoja na mwenzake Sony
Masamba wakisababisha mashabiki viuno vyao viweze kuzungushwa mithiri ya
feni.
Post a Comment