Tume
ya Uchaguzi (NEC) imemtangaza James Mbatia wa NCCR Mageuzi kuwa mbunge
mteule wa jimbo la Vunjo huku kada wa Chadema, Anthony Komu naye
akiibuka mshindi katika jimbo la Moshi Vijijini lililokuwa linaongozwa
na Waziri wa zamani wa Biashara na Viwanda, Dk. Cyril Chami kupitia CCM.
Akitangaza
matokeo ya majimbo hayo mawili mkoani Kilimanjaro kuamkia leo,
msimamizi Fulgence Mponji, amesema Mbatia amepata kura 60,187
akiwashinda wapinzani wake; Innocent Shirima wa CCM aliyepata kura
16,617 na Augustine Mrema wa TLP aliyepata kura 6,416.
Kutokana
na matokeo hayo, Mrema ameshindwa kutetea kiti chake cha ubunge katika
jimbo la Vunjo huku wananchi wa eneo hilo wakiendeleza historia ya
kutomchagua mbunge wa chama kimoja kwa vipindi viwili tangu kurudi kwa
mfumo wa siasa za vyama vingi.
Kwa
upande mwingine, CCM imepoteza jimbo la Moshi Vijijini kupitia kwa
mgombea Cyril Chami na kurudi tena upinzani baada ya kada wa Chadema,
Anthony Komu kutangazwa mshindi. Hata hivyo, waziri huyo wa zamani wa
Viwanda na Biashara hakuwepo wakati NEC wa kusaini kuonyesha kuwa
amekubali matokeo.
Kwa
mujibu wa Mponji, mbunge mteule wa Moshi Vijijini, Komu amepata kura
55,813 huku Dk Cyril Chami akijikusanyia kura kura 24,415.
Post a Comment