Mkurugenzi
wa NMB - Ineke Bussemaker (katikati) akizungumza na Wajumbe wa Jukwaa
la Wahariri Tanzania (Tanzania Editors Forum) jijini Dar es Salaam jana
kuhusu maadhimisho ya miaka 10 ya benki hiyo tangu ilipobinafsishwa na
hatua ilizopiga katika maendeleo ya benki.
Wajumbe
wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (Tanzania Editors Forum) wakimsikiliza
kwa makini Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker (katikati)
jijini Dar es Salaam jana kuhusu maadhimisho ya miaka 10 ya benki hiyo
tangu ilipobinafsishwa na hatua ilizopiga katika maendeleo ya benki.
Afisa
Mkuu wa Fedha wa Benki ya NMB, Waziri Barnabas (kushoto) akizungumza na
Wajumbe wa Jukwaa la Wahariri Tanzania jana kwenye makao makuu ya NMB.
Mkurugenzi
Mkuu wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker (kushoto) na Wajumbe wa Jukwaa
la Wahariri Tanzania (Tanzania Editors Forum) wakiangalia filamu fupi
kuhusu maadhimisho ya miaka 10 ya benki ya NMB tangu ilipobinafsishwa na
hatua ilizopiga katika maendeleo yake jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi
wa NMB – Ineke Bussemaker akisalimiana na Mhariri na Mmiliki wa ABM FM
ya Dodoma – Abdallah Majura kwenye mkutano kati ya NMB na Jukwaa la
Wahariri.
Mratibu wa Jukwaa la Wahariri – Prisca Kabendera akielezea kuhusu Jukwaa la wahariri na shughuli inazofanya.
Benki
ya NMB jana ilianza maadhimisho ya miaka 10 tangu kubinafsishwa huku
ikiweka bayana mafanikio makubwa iliyoyapata ikiwemo kuongeza matawi
kutoka chini ya 100 miaka 10 iliyopita mpaka matawi 173 leo hii, kutoka
kutokuwa na ATM mpaka ATM zaidi ya 600 na wateja kufikia zaidi ya
milioni 2 kutoka laki 6 miaka 10 iliyopita.
NMB
pia imefanikiwa kuwa na matawi katika kila wilaya nchini. Hii inaonesha
ni jinsi gani Benki imekuwa kwa kasi na kuwa benki namba moja kwa ukubwa
na faida kuliko benki nyingine yoyote nchini Tanzania.
Kwa
miaka 10 pia NMB imetumia zaidi ya shilingi Bilioni 7 kusaidia shughuli
za maendeleo ya jamii ikiwemo kusaidia madawati mashuleni, vifaa vya
hospitali katika hospitali mbalimbali za serikali huku ikichangia
kuongeza ufanisi wa utoaji huduma katika sekta ya afya na elimu.
NMB
Pia imechangia zaidi ya Bilioni 365 ndani ya miaka 5 tu fedha ambayo
imechangia sana kwenye bajeti ya serikali na hivyo kutumika kwa
maendeleo ya watanzania. Huo ni mchango mkubwa kuliko benki yoyote
nchini.
Kwa hisani ya Michuzi Blog
Post a Comment