Zetrida
Ezekiel ni mwanamuziki mahiri wa muziki wa injili aishiye mkoani
Kigoma, amekuwa mwanamuziki wa nyimbo za injili ambaye ni mwana kwaya wa
kikundi maarufu na kikongwe cha nyimbo za injili cha MKE MWEMA cha
mjni Kigoma. Zetrida ameolewa na ni mama wa watoto wanne, wa kike wawili
na wa kiume wawili.
Lakini baada ya kupata rai nyingi na kwa muda mrefu toka kwa wachungaji wake na watu mbali mbali kuwa atengeneze albamu yake kama mwanamuziki wa kujitegemea,hatimae mwezi wa August mwaka huu Zetrida alikuja Dar es Salaam na kuanza kazi ya kutengeneza albam yake binafsi.
Lakini baada ya kupata rai nyingi na kwa muda mrefu toka kwa wachungaji wake na watu mbali mbali kuwa atengeneze albamu yake kama mwanamuziki wa kujitegemea,hatimae mwezi wa August mwaka huu Zetrida alikuja Dar es Salaam na kuanza kazi ya kutengeneza albam yake binafsi.
Zetrida Ezekiel akiwa katika pozi.
Album yake inayoitwa Ringa na Yesu ina nyimbo nane na nyimbo zote amezifanyia Tika records chini ya mtayarisha muziki maarufu nchini aitwaye Ephraim Kameta ambapo nyimbo sita katika albam yake hiyo zilitengenezwa na Kameta na mbili zikitengenezwa mtayarisha muziki machachari PG zote katika studio za Tika records pia. Katika albam hiyo kuna nyimbo kama Ringa na yesu liyobeba jina la albam Malaika, waombee maadui zako na nyingine nyingi zenye kiwango cha hali ya juu.(P.T)
Akiongea
na mtandao huu kwa njia ya simu Zetrida alipoulizwa ana mipango gani ya
kufanya video ya albam hiyo Zetrida alisema "Natamani sana hata leo
nianze kuandaa video lakini pesa inagomba kwa saa hasa baada ya kutoka
kuandaa albam hii ya audio ambaye imechukua pesa nyingi kuandaa, inabidi
nijpange tena kwanza"
Na
alipoulizwa nini mipango yake ya baadae baada ya lutoa albamhiyo alisema
"Mipango yangu ya baadae ni kumtangaza Yesu ndani na na nje ya Tanzania
kwa kuwa ni kitu kilicho ndani ya damu yangu" Pia alielezea changamoto
alizokutana nazo wakati akitayarisha albam hiyo ni pamoja kutofanya kazi
kwa wakati uliopangiwa jambo ambalo hutokana na sababu mbali mbali
ikiwemo katikizo la umeme, ambapo inatokea kazi iliyokuwa ifanyike jana
inahamishiwa leo na wa leo ama utafanya kazi mida mibaya au kupangiwa
siku nyingine. Lakini nashukuru sana kuwa nimeeza kumaliza albam hiyo
bila tatizo.
Mwisho
kabisa Zetrida alipenda kutoa shukurani zake akisema "Napenda kumshukuru
Mungu kwa kunipa ujasiri wa kufanya albam yangu mwenyewe na pili mume
wangu kwa kuniruhusu kufanya kazi hii ya uimbaji pia kujitoa kwake kwa
hali na mali, vile vile bila kumsahau Mchungaji Joseph Malumbu wa
Kijichi Mtongani ambaye alihusika katika usimamaizi wa albam ya Ringa
kwa Yesu. Pia niwaombe tu wapenzi wa muziki wa injili waipokee albam
yangu na wainunue kwa wingi kwani humo kuna nyimbo nzuri sana zenye
kumtukuza Bwana Yesu hivyo kila mmoja ajipatie nakala yake sasa kwani
tayari albami ipo madukani.
Kwa mialiko popote ndani na nje ya Tanzania wasiliana naye kwa nambari
+255675 406917/ +255756823477
au kwa barua pepe
Post a Comment