Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

BREAKING NYUZZ... RAIS AMEMTEUA MHE.KASSIM MAJALIWA KUWA WAZIRI MKUU

Hatimaye Waziri Mkuu Mh. Kasim Majaliwa apendekezwa na Rais kisha kupigiwa kura na wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwenye Ukumbi wa Bunge Makao Makuu ya Tanzania, Dodoma, leo tarehe 19 November 2015.

Katibu karejea na mpambe wa Rais (ADC) anaingia na bahasha aliyotumwa na Rais kumletea Spika. Spika anafungua Bahasha tatu na anatangaza kuwa Rais amemteua Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu


Spika anasema barua imeandikwa na Rais kwa mkono wake mwenyewe haikuchapishwa.


Spika anasoma; '' Job Ndugai, Mh Spika, mimi mwenyewe kwa nafasi yangu kama Rais wa JMT nimemteua Mbunge wa Ruangwa mh. Kassim Majaliwa kuwa waziri mkuu wa JMT.''
Mhe. Kassim Majaliwa mbunge wa jimbo la Ruangwa jina lake limependekezwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli ambapo atapigiwa kura na wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Spika amesitisha Bunge kwa muda wa dakika 45.
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top