Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

MAHAFALI YA SHULE YA GAMALIEL YAFANA JIJINI MBEYA

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya pamoja naviongozi wa meza kuu wakiwa wamesimama kujiandaa na zoezi la kutoa vyeti kwa wahitimu.

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya akitoa cheti kwa mmoja wa wahitimu wa Mahafali ya pili ya Top Class

Mhitimu wa Top Class akiondoka na cheti huku akitabasamu

Baadhi ya Wahitimu wakionesha vyeti vyao
Mkuu wa wilaya ya Mbeya Nyirembe Munassa akiangalia ramani ya shule ya Gamaliel

Mkuu wa wilaya ya Mbeya Nyirembe Munassa akipokea maua kutoka kwa wanafunzi wa  The Gamaliel ilipofanya mahafali ya wanafunzi kuingia darasa la kwanza

Mkuu wa wilaya ya Mbeya Nyirembe Munasa akisalimiana na viongozi wa kimila wa maeneo ya Lyoto ilipo shule ya Gamaliel


DC Munasa akiweka saini kwenye kitabu cha wageni cha shule ya Gamaliel kabla ya kuanza kwa sherehe za mahafali ya darasa la kwanza la shule hiyo


Mkuu wa Wilaya ya Mbeya akivishwa Shada kama ishara ya kukaribishwa kwenye mahafali ya pili ya Top class ya Shule ya Gamaliel


Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Gamaliel wakishangilia kwa kupiga makofi kwenye mahafali ya shule hiyo mwishoni mwa wiki.

Wahitimu wa shule ya awali wanaotarajia kuingia darasa la kwanza kwenye shule ya Gamaliel

Mkuu wa wilaya ya Mbeya Nyirembe Munasa akiteta jambo na Mkurugenzi wa shule ya Gamaliel

Baadhi ya wanafunzi wa darasa la tatu wa shule ya Gamaliel wakiimba wimbo kwenye mahafali ya wanafunzi wanaoingia darasa la kwanza mwishoni mwa wiki
Baadhi ya wazazi na wageni mbali mbali wakiwa kwenye sherehe za Mahafali.
 
 
MKUU wa Wilaya ya Mbeya, Nyerembe Munasa amewataka wamiliki wa Shule binafsi kuwa na maono ya kupanua wigo wa utoaji wa elimu ili kuleta ushindani wenye tija kwa Taifa.
 
Mkuu huyo wa Wilaya alitoa rai hiyo hivi karibuni katika sherehe za Mahafali ya Pili ya Chekechea (top class) ya Shule ya Msingi na awali ya Gamaliel iliyopo Lyoto jijini Mbeya.
 
Nyerembe alisema elimu ni jambo muhimu katika maendeleo ya taifa lolote duniani hivyo ni wakati muafaka kwa wamiliki wa shule binafsi kuwekeza katika kutoa elimu yenye ushindani bila kuogopa.
 
“ Napenda nitoe wito sasa kwa wamiliki wa shule hii baada ya kuwa na madarasa ya awali na Msingi fikirieni kuanzisha shule ya Sekondari na baadaye Chuo ili watoto wanaotoka hapa waweze kuwa na mwendelezo mzuri kutokana na misingi waliyokulia” alisema Mkuu huyo wa Wilaya.
 
Aliongeza kuwa ili waweze kufanikisha hayo ni vema uongozi ukawa na malengo makubwa  hususani kuweka uwekezaji katika ufundishaji wa masomo ya sayansi ili kufikia matarajio ya Serikali kuwa na wataalamu wengi wa sayansi.
 
Alisema pia uongozi wa Shule hiyo unapaswa kuzingatia lishe kwa wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo kutokana na kuwa na umri mdogo ili waweze kukua wakiwa na afya imara itakayowasaidia kushika vizuri masomo yao.
 
Kwa upande wake Mkuu wa Shule hiyo, Edward Olesaka  alisema Wazazi wasiwe na shaka juu ya uwepo wa watoto wao shuleni hapo kwani elimu wanayoipata ni bora kwa kuwa walimu wanazingatia majukumu yao kikamilifu.
 
Naye mmoja wa Wakurugenzi wa Shule hiyo, Subilaga Mwambeta alisema ushauri uliotolewa na Mkuu wa Wilaya utaanza kufanyiwa kazi ambapo hivi sasa shule hizo zimeshaanza kupata usajili kutoka Serikalini.
 
Alisema ushirikiano ambao Serikali inaonesha katika shule binafsi unazidi kuwapa nguvu ya kupanua wigo wa utoaji wa elimu kwa watanzania.
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top