Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

MALISA JJ-MGAWANYO WA VITI MAALUMU; VIJANA WATENDEWE HAKI.!






Muda mfupi ujao Bunge la 11 litaanza vikao vyake rasmi mjini Dodoma baada ya wabunge wake kuapishwa. Idadi ya wabunge inayokadiriwa kuwemo katika bunge lijalo ni 396 kutoka vyama mbalimbali.

Vyama vyenye uwakilishi wa wabunge kupitia majimbo mwaka huu ni CCM (182), CUF (39), CHADEMA (35), ACT (1), na NCCR (1). Hata hivyo majimbo 8 hayakufanya uchaguzi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo vifo vya wagombea, hivyo watafanya uchaguzi mdogo baadae mwaka huu.

Wabunge wengine watatoka Baraza la Wawakilishi (5), Uteuzi wa Raisi (10), Mwanasheria Mkuu (1), Spika wa Bunge kama hatakuwa Mbunge (1), na wabunge wa viti maalumu.

Katika Viti Maalumu mgawanyo uliotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kutokana na uwiano wa kura za Urais na Ubunge kwa kila chama ni kama ifuatavyo. CCM viti 63, CHADEMA viti 43, CUF viti 7, NCCR viti 0 na ACT viti 0.

Kila chama kina utaratibu wake wa kuwapata wabunge wa viti Maalum kutokana na vigezo walivyojiwekea. CHADEMA kwa mara ya kwanza itapanda kutoka viti maalumu 25 bunge lililopita hadi viti 43 bunge hili. CCM imeporomoka kutoka viti maalum 86 bunge lililopita hadi wabunge 63 bunge hili.
Hii ina maana tunategemea vuguvugu jipya la mawazo ktk bunge lijalo kuliko ilivyokua ktk bunge lililopita. Ongezeko la wabunge wa upinzani ktk bunge lijalo ni dalili njema kwa wananchi kwamba bunge hili halitakuwa tena na zile "NDIOOO" zinazokera kwa sababu CCM peke yao hawataweza kufanya maamuzi. 

Nguvu ya upinzani ktk bunge lijalo ni kubwa na inaweza kuzima kelele za wabunge wa CCM pale inapofikia hatua ya kufanya maamuzi.

Hii ina maana nguvu ya vijana ktk bunge lijalo inahitajika sana kuliko wakati mwingine wowote. Kwa bahati mbaya vijana wengi waliogombea ubunge mwaka huu wamedhulumiwa haki yao hata pale waliposhinda kihalali kwa kura.

Kwa mfano jimbo la Kwela Daniel Naftal alishinda lakini akanyanganywa ushindi mezani, jimbo la Shinyanga mjini Kamanda Patrobas Pascal alishinda lakini akafanyiwa mizengwe, jimbo la Vwawa karatasi za majumuisho zilionesha Fanuel Mkisi ndiye Mshindi lakini akatangazwa mgombea wa CCM.

Hawa ni baadhi ya vijana ambao wangepata fursa ya kuwepo bungeni wangeibua vuguvugu la ujenzi wa hoja imara na zenye maslahi kwa taifaa kama ilivyokuwa kwa kina Kafulila, Mkosamali, Wenje etc.

Kwahiyo kupoteza vijana hawa na wengine kama hawa ni kupunguza sauti ya vijana bungeni. Hivyo basi ni busara vyama vikaona namna ya kurudisha sauti ya vijana kupitia wabunge wa viti maalumu.

Wapo wanawake vijana wenye uwezo mkubwa wa kujenga hoja na wenye historia ya kupigania maslahi ya umma bila kuhofu nguvu ya dola na vitisho vingine. Hawa ni vijana wanaopaswa kutizamwa kwa jicho la pekee na wapewe fursa ya uwakilishi ktk bunge lijalo.

Najua vipo vigezo vya chama kuwapata wabunge wa viti maalumu lakini ni vema vigezo hivyo vitizame pia nafasi ya vijana. Kutumia vigezo "general" tu kwa kila mtu ni kuwanyima fursa vijana wanaostahili.

Kwa mfano mwaka 2010 CHADEMA kilitumia kigezo cha wanawake waliogombea majimboni wakakosa ndio waliopewa kipaumbele kwny viti maalum. Lakini "approach" hii iliibua changamoto kadhaa baada ya baadhi ya wabunge akiwemo Leticia Nyerere na Chiku Abwao kupingana na misimamo ya chama hadharani.

Kwa hiyo ni vzr kigezo cha kugombea jimboni kisiwe kigezo pekee cha kuwapa nafasi wanawake, pawepo na vigezo vingine vyenye tija.

Kwa mfano ktk nafasi 43 walizopewa CHADEMA, nafasi 10 zinaweza kutengwa kwa ajili ya wanawake vijana waliofanya kazi kubwa ya kukijenga chama na kupigania maslahi ya umma kwa nyakati tofauti. 

Wapo vijana wengi wanawake waliofanya kazi kubwa ndani na nje ya chama lakini leo niwataje watano kama kielelezo cha wengine;

1. Pamela Maassay
Huyu binti hodari na msomi ambaye kwa muda mrefu amekuwa akitumia muda wake kwa shughuli za chama. Kitaaluma ni Mhandisi (Engineer) na Mjumbe wa Baraza Kuu la chama.

Alikua Mbunge wa bunge maalumu la Katiba akiwakilisha taasisi ya vijana lakini aliondoka bungeni na kuyakataa mamilioni ya shilingi baada ya kuona Rasimu ya Warioba iliyokua imebeba maoni wananchi ikitupiliwa mbali. 

Jambo hili lilimpa ushujaa mbele ya jamii ya kitanzania kwani ni vijana wachache wa umri wake wenye uwezo wa kukataa posho ya mamilioni ili kutetea maslahi ya umma.

Ndani ya chama ni kiongozi wa vijana jimbo la Kawe kwa Halima Mdee, na kabla ya hapo alikua kiongozi wa vijana jimbo la Ubungo. Ametumia majukwaa ya kisiasa kukijenga chama na kukipigania ktk mambo mbalimbali.

Pamela ni miongoni mwa vijana walioamua kuzunguka nchi nzima kwa kutumia rasilimali zao wenyewe ili kuwanadi wagombea ubunge wa CHADEMA katika majimbo mbalimbali. BUNGE LA 11 HALIPASWI KUMKOSA MTU HUYU.!

2. Nusrat Hanje
Huyu huwa namuita "Extra Ordinary Political Orator". Kati ya wanawake wachache wenye akili nyingi sana nchini ni binti huyu. Kwa wale ambao wamewahi kumuona "Live" ktk majukwaa ya kisiasa au wamewahi kumsikiliza ktk radio au Televisheni watakubaliana nami kuwa huyu binti ana kipaji cha pekee.

Ni mjenzi mzuri wa hoja, mwenye uwezo wa ushawishi na msemaji mzuri ktk hadhara (good public speaker). Kitaaluma ni Mwalimu lakini ameamua kuiacha kazi yake ili kufanya shughuli za chama.

Katika uchaguzi mkuu mwaka huu amefanya mikutano zaidi ya 50 akiwanadi wagombea ubunge na udiwani ktk mikoa karibu yote ya Tanzania bara. BUNGE LA 11 HALIPASWI KUMKOSA MTU HUYU.!

3. Upendo Peneza
Kati ya wanawake vijana waliowahi ku-inspire maelfu ya Watanzania ni Upendo hasa ktk mchakato wake wa kugombea uongozi wa Baraza la vijana mwaka jana.

Licha ya kwamba kura hazikutosha lakini aliacha alama kubwa ya heshima ktk mioyo ya watanzania. Miongoni mwa watu waliovutwa na uwezo wa huyu binti ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Mhe.Regunald Mengi ambaye alieleza kupitia ukurasa wake wa Tweeter kumuunga mkono Peneza.

Licha ya umri wake mdogo lakini ana uwezo mkubwa wa kujieleza, kushawushi na kujenga hoja. Amefanya kazi nyingi za kijamii zinazompa heshima kubwa nje na ndani ya chama.

Kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu Upendo alitangaza nia jimbo la Geita Mjini lakini kura hazikutosha. Licha ya kutopata nafasi hiyo lakini aliendelea kushiriki ktk kuwanadi na kuwaombea kura wagombea wa Ubunge na Udiwani jimbo la Geita na majimbo mengine ya kanda ya ziwa. BUNGE LA 11 HALIPASWI KUMKOSA MTU HUYU.!

4. Jesca Kishoa
Siasa zingekuwa muziki basi huyu tungesema "Bob Marley" au "Senzo" walivyo na heshima ktk muziki wa Reggae ndivyo ilivyo kwa Kishoa ktk siasa. Kazi alizofanya kwa ajili ya ujenzi wa chama zimempa alama ya heshima ktk maeneo mbbalimbali nchini. 

Lakini pia changamoto alizowahi kupata kwa ajili ya chama hazihesabiki. Amewahi kusimamishwa masomo mara kadhaa akiwa chuo kikuu kwa ajili ya siasa. Ameshiriki siasa za majukwaani tangu akiwa shuleni.

Ametembea maeneo mengi ya nchi hii kukijenga chama na kufundisha vijana ujasiri ktk kutetea maslahi ya umma. Ni mke wa Mhe.David Kafulila aliyekuwa Mbunge wa Kasulu.

Ktk uchaguzi mkuu mwaka huu Jesca aligombea Ubunge jimbo la Iramba Mashariki kwa Mwigulu Nchemba. Japo kura hazikutosha lakini alionesha dunia kuwa wanawake wanaweza.

Ikumbukwe Jesca alikua anagombea Ubunge akiwa ametoka tu kujifungua. Alikua anakwenda kwenye kampeni na mwanae kwenye gari. Huu ni ujasiri wa ajabu aliouonesha na hakika anastahili pongezi. 

Licha ya kugombea na Mwigulu Nchemba aliyekua waziri kwny serikali ya JK lakini Jesca hakuogopa uwaziri wa Mwigulu. BUNGE LA 11 HALIPASWI KUMKOSA MTU HUYU.!

5. Rose Mayemba
Huyu huwa namuita "The Iron Lady" kwa sababu kiumri ni mdogo, kiumbo pia ni mdogo lakini kiakili ni mkubwa sana. Ana akili kubwa kuliko umri wake. 

Kitaaluma ni Mfamasia anayefanya kazi serikalini. Amewahi kusimamishwa kazi mara kadhaa kwa ajili ya chama. Huyu ni miongoni mwa watu wachache waliohakikisha CHADEMA inakua na kushika hatamu mkoa wa Njombe, Iringa na Mbeya kwa nyakati tofauti.

Huwezi kuzungumzia ukuaji wa CHADEMA Nyanda za juu kusini bila kumtaja Rose Mayemba. Alikua Mwenyekiti wa CHADEMA Tawi la Chuo Kikuu RUCO wakati akisoma chuoni hapo.

Lakini hata baada ya kumaliza masomo na kuajiriwa bado anatumia muda wake mwingi kufanya shughuli za chama. Mwaka jana alishiriki kikamilifu kwny uchaguzi wa serikali za mitaa na akahakikisha tunapata nafasi nyingi za uongozi.

Hata baada ya kushinda aliandaa semina elekezi kwa gharama zake mwenyewe "akawatrain" viongozi wote wa serikali za mitaa waliochaguliwa.

Kwenye uchaguzi mkuu mwaka huu alitia nia ya kugombea Ubunge jimbo la Njombe kusini lakini kura hazikutosha. Licha ya kura kuwa hazikutosha lakini hakukata tamaa wala kurudi nyuma. Aliendelea kupigania chama na kuwanadi wagombea ubunge na udiwani ktk majimbo mbalimbali ya mkoa wa Njombe na nje ya mkoa wa Njombe. BUNGE LA 11 HALIPASWI KUMKOSA MTU HUYU.!

6. Asia Msangi
Kitaaluma huyu ni Mwanadiplomasia lakini ni mwanasiasa hodari. Ameshiriki kazi nyingi za kijamii nje na ndani ya chama. Ni miongoni mwa mabinti wadogo ndani ya CHADEMA lakini wenye uwezo mkubwa sana kichwani.

Kati ya watu waliojitolea kwa vitendo kuikuza CHADEMA jimbo la Ukonga na maeneo mbalimbali ya Dar ni pamoja na Asia. Amechangia vifaa vya uenezi ktk majimbo mbalimbali, ameshiriki kutoa mafunzo sehemu mbalimbali, amefanya mikutano ya hadhara maeneo mengi akikinadi chama.

Kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu alitia nia ktk jimbo la Ukonga lakini kura hazikutosha. Hata hivyo aliendelea kukipigania chama akiwanadi wagombea udiwani na ubunge waliopitishwa. Huyu ndiye aliyekuwa Kampeni meneja wa Mbunge wa Ilala aliyedhulumiwa Muslim Hassanali. BUNGE LA 11 HALIPASWI KUMKOSA MTU HUYU.!

NB: Kama nilivyotangulia kusema awali kuwa wapo wengi wenye sifa na uwezo lakini hawa ni wachache wanaowakilisha kundi la wanawake vijana wenye sifa za kuwa Wabunge katika bunge lijalo. Ni muhimu chama kisipuuze sauti za vijana kwenye mchakato huu wa kuwapata wawakilishi wetu kupitia viti maalumu. 


#‎BUNGE‬ LA 11 HALIPASWI KUWAKOSA WATU HAWA.
Kumbuka hapa nazungumzia vijana. Post hii ni dedication kwa vijana wote ndani ya chama waliofanya kazi kubwa kukikuza chama. Najua wapo wanawake wengine wenye sifa na uwezo lakini si vijana maana are more than 35 years old. So kuwa makini unapocoment,, kumbuka hoja hapa ni WANAWAKE VIJANA WENYE UWEZO.

Alamsiki,
©Malisa GJ,
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top