Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

NAIBU SPIKA AANZA KWA KUONJA JOTO LA JIWE



Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson, amekalia kiti hicho kwa kuanza kuonja 'joto la jiwe' baada ya kushindwa kujibu swali lililomtaka aeleze muda gani aliojiunga na Chama cha Mapinzuduzi (CCM) huku akikumbana na zomea zomea kali kutoka kwa wabunge wa vyama vya upinzani.


Mtafatuku huo uliibuka ndani ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma jana, wakati Dk. Tulia alipokuwa akijinadi kwa wabunge kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi wa Naibu Spika.


Nafasi hiyo ilikuwa ikiwaniwa pia na Mbunge wa Kaliua (Cuf), Magdalena Sakaya, ambaye kura 101 alizopigiwa hazikutosha kumfanya akalie kiti hicho dhidi ya Dk. Tulia aliyepata kura 250.


Hata hivyo, swali lilosababisha bunge hilo kuvurugika lilitoka kwa Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko (Chadema), ambaye alimtaka Dk. Tulia atoe ufafanuzi muda wa uanachama wake ndani ya chama hicho, na kama mtumishi wa serikali ataje siku aliyotangaza kuachia ngazi na kujiunga na CCM kwani sheria na kanuni za utumishi wa serikali inamzuia kujiunga na chama chochote cha siasa.


?Nakuomba utulieleze sisi wabunge kwa kuwa wewe ulikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali na kwa mujibu wa sheria inafahamika wazi kuwa mtumishi wa serikali hasa katika ngazi yako hukutakiwa kuwa mwanachama wa chama cha siasa. Tunaomba utuambie lini ulijiunga na CCM, hasa kwa ukizingatia hivi karibuni ulisimamia kesi ya mita 100,? aliuliza Matiko.


Swali hilo lilimfanya Spika Job Ndugaye ambaye alikuwa akiendesha kikao hicho kuwauliza wabunge kama linafaa kujibiwa. Wabunge hasa wa upinzani walijibu kwa sauti kwamba hilo ni swali na linapaswa kujibiwa.
?Mheshimiwa Dk. Tulia haya jibu swali hilo,? Ndugai alimtaka kujibu.


Dk. Tulia wakati akijibu alionekana kutumia muda mwingi kufafanua vifungu vya katiba na sheria vinavyozungumzia zuio hilo, jambo ambalo wabunge wa kambi ya upinzani walionekana kutoridhika nalo.


?Kama ulivyosema mimi ni mwanasheria, katiba nimeisoma, sheria zinazozungumzia utumishi wa umma nimezisoma na kanuni zake nimezisoma?nasema hivi kanuni nimezisoma, sheria nimezisoma,? alisema na kukatishwa na sauti za wabunge zikimtaka kujibu swali.


Kutokana na hali hiyo, Spika Ndugai aliingilia kati kwa kuwaomba wabunge kuacha kumzonga mgombea na vizuri wangemsikiliza kama walivyofanya wakati Sakaya akijinadi.


?Mheshimiwa spika yapo makundi matatu ya watumimishi wanaokatazwa kuwa wanachama na vyama vya siasa, kwanza ni wanajeshi ambao ni polisi na wanao?,? alijibu Dk. Tulia na kukatishwa na zomeazomea kutoka kwa wabunge.


Hata hivyo, Spika Ndugai alisimama na kumuamuru Katibu wa Bunge kuendelea na taratibu za uchaguzi.
Baada ya uchaguzi, Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashilillah, alimtangaza Dk. Tulia mshindi baada ya kupata kura 250 sawa na asilimia 71.2 wakati Sakaya akipata kuta 101 ambazo ni sawa na asilimia 28.8 za kura zote.
Alisema wabunge wote waliosajiliwa walikuwa 369, lakini idadi ya waliopiga kura ni 351.



Kutokana na matokeo hayo, Spika Ndugai alimtangaza Dk. Tulia kuwa Naibu Spika wa Bunge hilo na kumuapisha rasmi kuanza kazi yake hiyo mpya.
WATUMIA BUSARA


Baada ya kutangazwa matokeo, Dk. Tulia na Sakaya walitumia busara kupoza mvutano huo kwa kila mmoja kutaka udumishwe umoja na mshikamano katika kutekeleza kazi za chombo hicho kwa kusimamia, kuwajibisha na kuishauri serikali.


CHANZO: NIPASHE
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top