Mkuu
wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange (wa pili kulia), Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini, Ernest Maangu (wa tatu kulia) na Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam, Said Sadick wakipiga saluti ulipokuwa unaimbwa wimbo
wa Taifa wakati wa mazoezi ya sherehe za kuapishwa Rais wa Awamu ya
Tano, Dk John Magufuli kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Askari wa Jeshi la
Wananchi akiigiza kama Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini, Jenerali Davis
Mwamunyange na mwingine akiigiza kama Rais anayemaliza muda wake, Jakaya
Kikwete wakati wa mazoezi ya sherehe za kuapishwa Rais wa Awamu ya
Tano, Dk John Magufuli kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Maofisa mbalimbali
wakiwa katika kibanda cha kiapo wakipanga jinsi viongozi watakavyokaa
wakati wa sherehe za kuapishwa Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli
kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Kikundi cha sarakasi kikitumbuiza wakati wa maandalizi hayo
Wasanii kutoka Zanzibar wakicheza ngoma ya kibati wakati wa mazoezi hayo
Mtu aliyeigiza kama
Rais Jakaya Kikwete, akiwa amesimama alipokuwa akipigiwa mizinga ikiwa
ni ishara ya kuagwa kwa rais huyo kabla ya kuapishwa Rais mpya wa Awamu
ya Tano, Dk John Magufuli wakati wa mazoezi hayo.
Viongozi mbalimbali wakiwemo wa vyombo vya ulinzi na usalama wakiwa Jukwaa Kuu wakati wa maandalizi hayo.
Baadhi ya wananchi
wakiwa wamesimama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa na Bendi ya Jeshi la
Wananchi Tanzania (JWTZ) wakati wa maandalizi hayo.
Mtu aliyeigiza kama Rais
Jakaya Kikwete, akielekea kukagua gwaride la heshima la kumuaga wakati
wa mazoezi hayo.
PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Post a Comment