Mpango wa serikali wa elimu bure unaonesha kuwa serikali inatenga
shilingi elfu kumi (10,000) kwa mwaka mzima kwa kila mwanafunzi wa shule
ya msingi. Hiyo ina maana kwamba kila mwanafunzi anapelekewa shilingi
833 za kutumia mwezi mzima - kama shule ina wanafunzi 500 inapelekewa
shilingi 416,500 kwa mwezi.
Kama shule moja ina walinzi wawili na inawalipa shs 150,000 kwa mwezi mmoja ina maana fedha zinazotumwa zinaishia kwa
walinzi na kubakiza shilingi 116,500. Hizi zikitumika kulipa maji na
umeme haibakii hata senti tano. Nimeongea na baadhi ya walimu wakuu
wanasema wamechanganyikiwa na hawajui cha kufanya.
Sijui kama mahitaji ya shule zetu yamekamilika? Hebu serikali ijipange
zaidi ili tusije kuzua bomu jingine kwenye elimu. “Pump more money on
education”, hakuna njia nyingine!
Post a Comment