Serikali imedhamiria kulifufua upya
Shirika la Ndege nchini kwa kulinunulia ndege mpya na kulipa mtaji ili lifanye
kazi kibiashara na kutengeneza faida kama ilivyokusudiwa awali.
Akizungumza na menejimenti na wafanyakazi
wa Shirika hilo, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame
Mbarawa amesema kuwekeza kwenye shirika hilo kutaongeza fursa za kiuchumi
na kuvutia wasafiri wengi kufika nchini moja kwa moja na kuvutia sekta ya
utalii.
Pia waziri Mbarawa amewataka wafanyakazi
wa Shirika hilo ambao sio waadilifu na wavivu kuondoka mara moja ili kupisha
wafanyakazi wabunifu na wenye mawazo ya kibiashara kuendesha shirika hilo kwa
faida.
“Tunataka watu watakaolitoa shirika hili
kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa kuliwezesha kiuchumi na kujitegemea ili
kushindana na mashirika mengine ya ndege katika biashara“, amesisitiza Mbarawa.
Kwa upande wake Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa ATC, Johnson Mfinanga amemwambia Waziri Mbarawa kuwa kwa
sasa shirika hilo lipo katika hali mbaya kiuchumi na hivyo kuhitaji nguvu ya
Serikali kulikwamua ili litoe huduma inayostahili.
Post a Comment