Naibu wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) akipata maelezo machache
kutoka kwa Meneja uendeshaji wa Hospitali ya Sanitas, Bi. Gean Cabral
wakati walipowasilia katika ziara hiyo..
Dk Kigwangalla akikagua baaadhi ya sehemu katika hospitali hiyo.
Dk.
Kigwangalla akizungumza na baadhi ya wagonjwa (hawapo pichani) namna
Serikali ya Rais Magufuli inavyofanya kazi kwa kusimamia haki na usawa
ikiwemo kufika katika maeneo yenye kero na kuchukua hatua ilikumuokoa
Mwananchi katika kupata haki yake na huduma bora anayostahiki.
Dk. Kigwangalla akitoa maagizo hayo kwa Meneja uendeshaji wa hospitali hiyo, Bi. Gean Cabral
Dk. Kigwangalla akimuonesha moja ya 'karatasi' iliyoandikwa ujumbe
mbalimbali dhidi ya madai kutoka kwa wafanyakazi wa Hospitali hiyo.
Meneja Uendeshaji wa Hospitali hiyo Bi. Gean Cabral akifafanua jambo pamoja na Naibu Waziri wakati wa ziara hiyo.
Dk Kigwangalla akiangalia namna hali ya Maabara ya Hospitali hiyo
licha ya kuwa na vifaa vya kutosha, lakini imeshindwa kuweka mpangilio
mzuri unaotakiwa kutumika katika mahabara. ikiwemo suala la usafi.
Naibu Waziriwa Afya, Dk. Kigwangalla (kushoto), Msajili wa
Hospitali Binafsi pamoja na maafisa wengine akiwemo Mganga Mkuu wa
Wilaya ya Kinondoni, Dk. Aziz (kulia) wakijadiliana jambo muda mfupi
baada ya kumalizika kwa ziara hiyo ya kushtukiza kuangalia namna ya
uendeshaji katika huduma za Sekta za Afya, zikiwemo za Serikali na zile
za watu binafsi. (Picha zote na Andrew Chale,Modewjiblog/MO tv).
Naibu
wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.
Hamisi Kigwangalla ameagiza kufungwa mara moja Chumba cha upasuaji cha
hospitali ya Sanitas ya Mikocheni Jijini Dar es Salaam baada ya kubaini
kuwa na kasoro mbalimbali ikiwemo mfumo na ramani yake kimefungwa kwa
kutokidhi vigezo vya kimataifa vya namna chumba hicho kinavyotakiwa
kuwa.
Dk. Kigwangalla ametoa agizo hilo mapema jana Februari 29.2016,
alipofanya ziara ya kushtukiza kwenye hospitali hiyo majira ya saa nane
na nusu mchana ambapo baada ya kutembelea hospitali nzima na kushuhudia
namna ya utolewaji wa huduma, hakuridhishwa na hali aliyokutana nayo
kwenye chumba hicho na kutoa maagizo kwa Msajili wa Hospitali Binafsi,
Dkt. Pamela Sawa kufunga chumba hicho mpaka uongozi wa hospitali hiyo
utakapofanya marekebisho ya mapungufu yaliyopo.
“Chumba cha upasuaji hakiko sawa, siwezi kuvumilia kuacha chumba
hiki kiko chini ya kiwango cha kimataifa. Rekebisheni chumba hiki kwa
kutumia mfumo wa ramani wa wizara,” alieleza Dkt. Kigwangalla wakati wa
kutoa maagizo kwa mmoja wa Ofisa wa Hospitali hiyo.
Aidha uongozi wa hospitali hiyo umepewa siku saba wawe
wamewasilisha maelezo ya kutowalipa mishahara kwa kipindi cha miezi
minne watumishi wake pamoja na jinsi wanavyoteketeza taka hatarishi za
hospitali hiyo.
Katika ziara hiyo Naibu Waziri huyo alipata malalamiko kutoka kwa
watumishi hao ambao wamelalamikia kukatwa kwa makato ya mafao pasipo
kupelekwa mahali husika kwa zaidi ya miaka mitatu na nusu.
Dkt. Kigwangalla alivitaja viwango vya chumba cha upasuaji kuwa
kinatakiwa chumba cha kubadilishia mavazi,kunawa mikono,sehemu ya alama
maalum zenye rangi nyekundu, meza ya upasuaji, ukanda wa usafi, chumba
cha mapunziko baada ya kutoka kwenye upasuaji na chumba cha kusafishia
vifaa vya upasuaji na kuna mashine maalum kwa kuwa kila upasuaji una
idadi ya vifaa vinavyotumika.
Aliongeza kuwa viwango hivi vinawekwa ili kuepuka maambukizi.
Kwa upande wake Meneja Uendeshaji wa hospitali hiyo, Bi. Gean
Cabral alisema watarekebisha mapungufu yaliyobainika pamoja na kufanya
yale yote waliyoagiziwa baada ya tukio hilo.
Post a Comment