Serikali kupitia Waziri wa Habari,
Utamaduni, Wasanii na Michezo, wamewapongeza wasanii wa Tanzania kwa
kuipeperusha vyema Bendera ya Tanzania nje ya mipaka kwa kufanya vizuri
na kuibuka na ushindi ikiwemo tuzo katika filamu bora za Kiswahili
zinazotoka Tanzania.
Akitoa pongezi hizo mapema leo 7
Machi.2016, Waziri wa Habari, Mh. Nape Nnauye aliyetembelewa ofisini
kwake na wasanii mbalimbali wa filamu nchini waliowasindikiza washindi
wa tuzo hizo za African Magic Viewers’ Choice Awards (AMVCA2016)
zilizotolewa mwishoni mwa wiki nchini Nigeria,
Akiwemo mshaindi wa tuzo ya filamu
Bora ya Lugha ya Asili (Best Local Language -Swahili) kupitia filamu ya
‘Kitendawali’, Msanii Single Mtambalike ‘Rich Rich’ pamoja na Rais wa
Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF),Simon Mwakifwamba ambapo Waziri
aliwapongeza kwa mshikamano wao huo waliouonyesha na hata kurudi kutoa
pongezi.
Waziri Nape amebainisha kuwa, awali
Rich Rich kabla ya kwenda Nigeria, alipata Baraka kutoka kwake hivyo
hata kurejea kutoa shukrani ni jambo jema huku akieleza kuwa, Serikali
itahakikisha inawalea wasanii katika umoja pamoja na kuweka mazingira
mazuri ya ufanisi katika shughuli zao ikiwemo kuandaliwa Sera, kanuni na
misingi ya sharia katika kuifanya tasnia ya filamu kuwa ya kimataifa
zaidi na yenye kuleta fursa za ajira kwa wasanii ndani na nje.
“Kwa nafasi yangu ya Uwaziri.
Nitahakikisha nawapigania wasanii kufikia malengo tuliyoyakusudia. Hii
ni paamoja na kuwa na Sera madhubuti na kuzuia mianya ya wafujaji wa
kazi za Wasanii wa Tanzania. Serikali ya awamu ya tano kupitia kwa Rais
wetu Mh. Dk. John Pombe Magufuli ameanza na ili la stika za TRA
na munashuhudia wenyewe Mamlaka ya
Mapato inavyopambana na watu wanaorudisha maendeleo ya wasanii nyuma kwa
kufunga maduka yao huu ni mwanzo tutapambana mpaka mwisho katika hili”
alieleza Mh.Nape na kupaata pongezi kutoka kwa wasanii wenyewe ambao
waliweza kushangilia kwa kauli hiyo ya matumaini huku wakipiga makofi.
Aidha, katika tukio hilo, Serikali
imeweza kuwatunukia wasanii hao walioshinda tuzo hizo za AMVCA 2016
vyeti maalum vya shukrani hii ni pamoja na wasanii wote ambao filamu zao
pia zilienda kushindanishwa huko pamoja na waandaaji waliowezesha
filamu hizo kwa mchango wao mkubwa.
Katika tuzo hizo mbali na Rich
Rich, kushinad tuzo hiyo, Msanii mwingine aliyeshinda ni pamoja na
Msanii Elizabeth Michael (Lulu) akishinda tuzo ya Filamu Bora ya Afrika
Mashariki (Best Movie -Eastern Africa) kupitia filamu yake ya ‘Mapenzi’.
Post a Comment