Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

ANGALIA REKODI ZA JOSE MOURINHO DHIDI YA GUARDIOLA, WENGER, RANIERI, KLOPP, POCHETTINO NA CONTE

Mourinho vs other 3
Jose Mourinho ameteuliwa kuwa kocha wa mpya wa Manchester United na sasa akili zote za watu zina shauku ya kuona namna msimu ujao wa ligi ya England utakavyokuwa.
Kocha huyo wa zamani wa Chelsea, ameteuliwa kwa kazi maalum ya kuirejesha United kwenye mstari baada ya kuwa imepotea kwa takriban misimu mitatu mfululizo chini David Moyes na Louis van Gaal ambaye ametimuliwa hivi karibuni. Lakini licha ya ukweli kwamba Jose Mourinho anatambulika kuwa na ushawishi kwenye timu nyingi alizopita hivyo kuchagiza matokeo mazuri, lakini kibarua chake kipya hakitakuwa rahisi hata kidogo.
Mourinho anaenda kukumbana na changamoto kubwa sana. Anakutana tena na mpinzani wake wa La Liga Pep Guardiola anayekuja Manchester City, Arsene Wenger wa Arsenal na Claudio Ranieri wa Leicester. Pia kuna Jurgen Klopp wa Liverpool, Mauricio Pochettino wa Tottenham na bila ya kusahau Antonio Conte ambaye anakuja Chelsea.
Mtandao wa Sky Sports umetoa rekodi za head-to-head za Mourinho dhidi ya makocha wenzake vigogo wa Ligi ya England.
Mourinho v Guardiola
Uhasama kati ya Mourinho na Guardiola ulianza wakati akiwa Inter Milan, pindi walipokutana katika nusu fainali ya Champions League mwaka 2010 wakati huo Guardiola akiinoa Barcelona.
Baadaye msimu uliofuata Mourinho alijiunga na Madrid na kukaribishwa na kipigo cha mabao 5-0 kutoka kwa Barcelona iliyokuwa chini ya Guardiola, baadaye kupata ushindi wa 1-0 katika fainali ya Copa del Rey na kubeba ndoo.
Kwa ujumla, Guardiola ana rekodi nzuri mbele ya Mourinho pale timu zao zinakutana katika michuano tofauti. Kati ya michezo 16 waliyokutana Mourinho ameshinda michezo mitatu tu. Hivyo Mourinho atakuwa akipambana kuhakikisha anaondoa rekodi hiyo mbovu .
Mourinho v Wenger
Mourinho atakuwa na fursa nyingine ya kukutana na Arsene Wenger. Wawili hao wamekuwa wakiingia katika migongano ya vita ya maneno tangu mwaka 2004 na vita hiyo kufukia kilele kibaya mwaka 2014 pale wawili hao waliposhikana mashati wakati timu zao zikipambana kunako dimba la Stamford Bridge.
Katika suala zima la matokeo mazuri, Mourinho amemtawala sana mpinzani wake. Hajawahi kufungwa na Wenger katika michezo 13 ya ushindani. Kipigo kikubwa kabisa alichwahi kumpa Wenger ni kile cha magoli 6-0 katika dimba la Stamford Bridge wakati huo Wenger akiadhimisha kutimiza michezo 1000 akiwa kama kocha wa Arsenal.
Ushindi wa Arsenal wa bao 1-0 katika mchezo wa Ngao ya Jamii mwaka 2015, ulikuwa ndiyo pekee ambao Wenger anaweza kujivunia, lakini Mourinho bado atakuwa na shauku ya kutopoteza mchezo wowote wa ushindani dhidi ya mpinzani wake huyo na kuendeleza rekodi ya kutofungwa.
Mourinho v Klopp
Real Madrid chini ya Mourinho ilikutana na Borussia Dortmund ya Jurgen Klopp mara nne katika Ligi ya Mabingwa Ulaya katika msimu wa 2012/13. Katika michezo yote waliyokutana, Klopp aliibuka kidedea, akishinda michezo yake kwenye hatua ya makundi na vile vile kumtupa nje katika hatua ya nusu fainali, shukrani za pekee ziende kwa Robert Lewandowski ambaye alipiga zote nne.
Wawili hao pia walikutana Ligi kuu England mwaka jana ambapo Klopp akiwa na Liverpool aliiadhibu Chelsea ya Mourinho kwa mabao 3-1, katika mchezo uliofanyika Stamford Bridge.
Mourinho v Pochettino
 
Mourinho amekutana na Pochettino wakati akiinoa Espanyol mara wakati huo akiifundisha Real Madrid kati ya mwaka 2010 mpaka 2013. Katika michezo hiyo Mourinho alishinda mara nne na kutoa sare mara mbili.
Pia walikutana mara nne wakati Mourinho akiwa Chelsea na Pochettino akiwa Tottenham. Kwenye mchezo wao wa kwanza, Mourinho alishinda 3-0 na kumfunga katika fainali ya Capital One Cup. Lakini Mourinho alikuja kupata kipigo kitakatifu cha mabao 5-3 katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa kwenye dimba la White Hart Lane
Mwezi November mwaka jana, wawili hao walikutana tena na kutoa suluhu kabla ya Mourinho kutimuliwa Chelsea.
Mourinho v Ranieri
Mourinho alichukua mikoba ya Ranieri Chelsea mwaka 2004. Lakini iliwachukua takriban miaka minne pale walipokutana kwa mara ya kwanza msimu wa 2008/09. Mwaka huo, Mourinho wakati akiinoa Inter aliibuka na ushindi dhidi ya Juve ya Ranieri.
Katika msimu huo Juventus walimaliza katika nafasi ya pili, na Ranieri akaenda Roma. Mourinho wakati huo bado akiinoa Inter hakushinda kwenye michezo yote miwili ya Sirie A dhidi ya  Roma ya Ranieri, lakini alifanikiwa kumfunga 1-0 Ranieri katika fainali 1-0 ya kombe la Coppa Italia.
Miaka mitano baadaye wawili hao wanakutana Mourinho akiwa tena Chelsea huku Ranieri akiinoa Leicester. Wamekutana mara moja na Leicester kuifunga Chelsea kwa magoli 2-1 December mwaka jana. Huo ndiyo ulikuwa mchezo wa mwisho kwa Mourinho kabla ya kutimuliwa, na hatimaye Ranieri alifanikiwa  kubeba taji lake la kwanza akiwa nchini England.
Mourinho v Conte
Mourinho amekutana na Conte mara moja tu. Ilikuwa ni December mwaka 2009 wakati Inter ya Mourinho ilipomenyana na Atalanta ambayo ilikuwa chini ya Conte na mchezo kumalizika kwa matokeo ya sare ya 1-1. Baada ya hapo hawajawahi kukutana tena.
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top