Sasa ni dhahiri shahiri kwamba mwali anaelekea Jangwani njia ni nyeupe kwa wa 'Kimataifa' kuendelea kulikwea pipa tena msimu ujao wa Klabu Bingwa Afrika kwani Ubingwa ni Wao .
Azam Fc tayari wamenyoosha mikono juu baada ya jana kutoka sare ya 2-2 na JKT Ruvu. HUku pia wakongwe wengine Simba nao wakiwa hoi bila matumain yeyote kwa sasa hivyo njia ni nyeupe kwa Yanga na utaamini zaidi baada ya Viongozi wa Simba sasa kutoa maneno dhidi ya Yanga.
Kwa Matokeo
hayo yanamaanisha kwamba, Yanga wajitahakikishia kutetea taji hilo Mei
10 wakishinda dhidi ya Mbeya City Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, kwani
watafikisha pointi 71 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine ya Ligi
Kuu.
Sare hiyo inaifanya Azam FC ijiongezee pointi moja na
kufikisha 60 baada ya kucheza mechi 27 na inaweza kumaliza na pointi 69
ikishinda mechi tatu za mwisho, wakati Simba yenye pointi 58 inaweza
kumaliza na pointi 70 ikishinda mechi zake nne zilizobaki.
Katika
mchezo wa leo uliochezeshwa na refa Selemani Kinungai wa Morogoro
aliyesaidiwa na washika vibendera Lulu Mushin na Shaffih Mohammed wote
wa Dar es Salaam, hadi mapumziko Azam walikuwa mbele kwa mabao 2-0.
Mabao
hayo yalifungwa na pacha kutoka Ivory Coast, kiungo Kipre Michael Balou
dakika ya 31 na mshambuliaji Kipre Herman Tchetche dakika ya 37.
Kipindi
cha pili, JKT Ruvu inayofundishwa na gwiji wa soka nchini, Alhaj
Abdallah Athumani Seif ‘King Kibadeni’ ilibadilika na kufanikiwa
kusawazisha mabao yote mawili.
Alianza Mussa Juma kufunga kwa penalti dakika ya 56 na Najim Magulu dakika ya 72.
Kikosi
cha Azam FC; Aishi Manula, Erasto Nyoni, Gardiel Michael, Abdallah
Kheri, David Mwantika/Said Mourad dk46, Himid Mao, Kipre Balou/Khamis
Mcha ‘Vialli’ dk80, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Mudathir Yahya/Ramadhani
Singano ‘Messi’ dk64, John Bocco na Kipre Tchetche.
JKT Ruvu;
Madenge Ramadhani, Hamisi Seif, Omar Kindamba, Paul Mhidze, Renatus
Morris, Nashon Naftali, Abdulrahman Mussa/Samuel Kamuntu dk46, Hassan
Dilunga, Najim Magulu, Mussa Juma na Saad Kipanga/George Minja dk89.
Post a Comment