Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

HANS POPPE AMJIA JUU JERRY MURO

Wakubwa wanapogombana ujue kuna jambo haswa wakubwa wenyewe zikiwa ni klabu kongwe nchini Simba na Yanga.
 
Wote wanajuana nje na ndani ya uwanja.Namna timu hizi zinavyofanya fitna ili ziweze kupata matokeo mazuri katika mechi zao za Ligi lakini mara wanapofika katika mechi za kimataifa hali huwa tete sana mara nyingi huishia raundi ya pili.
 
Hivi karibuni Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba,Zacharia Hans Poppe ametoa mwanga kidogo kwa yale yanayofanyika kwa wakongwe hao wa soka nchini.Akimshutumu Msemaji wa Yanga Jerry Muro.
 
HIVI NDIVYO ALIVYOHOJIWA NA GAZETI LA CHAMPIONS:
 
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema ameshangazwa na Msemaji wa Klabu ya Yanga, Jerry Muro kujishitukia baada ya yeye kusema mwishoni mwa ligi, kuna michezo ya rushwa na akaitaja aina yake.
 
 


Hans Poppe amesema ameona Muro akihojiwa na baadhi ya vyombo vya habari na kusema anataka kumpeleka Takukuru ili akaeleze kuhusiana na rushwa.“Lakini kinachonishangaza ni kitu kimoja, mimi sikutaja jina la mtu wala timu. Utaona nilifanya mahojiano na gazeti la Championi, hata ilivyoandikwa sikutaja klabu wala jina la mtu, sasa unapomsikia mtu wa sehemu fulani anakurupuka na kusema kitu, huoni hii ni hofu.“Nimeshangazwa sana kusikia mtu anahojiwa, anajitaja, analalamika wakati hakuwa ametajwa mtu,” alisema Hans Poppe.“Hii inanikumbusha mwaka 1978, Uganda walikuwa wanarusha ndege zao za kivita zinaingia hadi anga ya Tanzania. Rais Nyerere akasema kuna watu ambao ni majirani zetu wanarusha ndege zao zinaingia ndani ya enero letu, nafikiri wanatutafuta.“Siku iliyofuata Iddi Amini aliyekuwa Rais wa Uganda wakati huo akasema, sio mimi. Sasa ndiyo anachofanya huyu kijana hapa,” alisema.
Hans Poppe alihojiwa na gazeti la michezo la Championi na kueleza kuhusiana na suala la rushwa.

author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top