Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kulia)
akizinduwa nembo mpya ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) pamoja na
kuzinduwa huduma ya mtandao wa kisasa wa 4G LTE leo jijini Dar es
Salaam. Kushoto ni Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Bi. Edwina
Lupembe akishiriki zoezi hilo. Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kulia)
akionesha nembo mpya ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) mara baada ya
kuizindua.
Kushoto ni Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Bi. Edwina Lupembe akishiriki zoezi hilo. Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kulia)
akimpongeza, Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk Kamugisha Kazaura (kushoto)
mara baada ya uzinduzi wa nembo mpya ya Kampuni ya TTCL pamoja na
uzinduzi wa huduma ya mtandao wa kisasa wa 4G LTE leo jijini Dar es
Salaam. Katikati ni Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Bi. Edwina
Lupembe. Ofisa
Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk Kamugisha Kazaura akiteta jambo na Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, katika hafla ya
uzinduzi wa nembo mpya ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) pamoja na
kuzinduwa huduma ya mtandao wa kisasa wa 4G LTE leo jijini Dar es
Salaam. Mwakilishi
wa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bi. Edwina
Lupembe akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa nembo mpya ya Kampuni ya
Simu Tanzania (TTCL) pamoja na kuzinduwa huduma ya mtandao wa kisasa wa
4G LTE leo jijini Dar es Salaam. Baadhi
ya maofisa wa kampuni ya TTCL pamoja na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kulia) wakifuatilia hotuba ya
Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Bi. Edwina Lupembe pamoja na
Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk Kamugisha Kazaura (hayupo pichani)
katika uzinduzi wa nembo mpya ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) pamoja
na kuzinduwa huduma ya mtandao wa kisasa wa 4G LTE leo jijini Dar es
Salaam. Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (wa pili
kulia) akijibu maswali ya wanahabari mara baada ya kuzindua nembo mpya
ya Kampuni ya TTCL pamoja na uzinduzi wa huduma ya mtandao wa kisasa wa
4G LTE leo jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Mwakilishi wa
Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Bi. Edwina Lupembe pamoja na Ofisa Mtendaji
Mkuu wa TTCL, Dk Kamugisha Kazaura (pili kushoto). Baadhi
ya maofisa waandamizi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) wakiwa katika
picha ya pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk Kamugisha Kazaura
(katikati) mara baada ya uzinduzi wa nembo mpya ya Kampuni ya TTCL
pamoja na uzinduzi wa huduma ya mtandao wa kisasa wa 4G LTE leo jijini
Dar es Salaam.[/caption] KAMPUNI ya Simu Tanzania (TTCL) imefanya
mabadiliko ya nembo yake pamoja na kuzinduwa huduma ya mtandao wa kisasa
wa 4G LTE ikiwa ni muendelezo wa mpango wa kufanya mabadiliko ya
kibiashara kwa kampuni hiyo. Nembo hiyo mpya ya TTCL na huduma ya 4G LTE
vimezinduliwa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa huku akiipongeza kwa hatua hiyo ya
kuleta mabadiliko ya kiutendaji na uwajibikaji unaolenga kuonesha tija
na ubora. Waziri Mbarawa alisema uzinduzi huo ni utekelezaji wa agizo la
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli la
kufanya kazi kwa bidii, maarifa, uadilifu na kufikia viwango vya juu
kabisa vya kutoa huduma kwa umma sambamba na mpango mkakati wa TTCL
kibiashara kwa kipindi cha mwaka 2016-2018. "Pamoja na pongezi hizi za
dhati, naomba mtambue kuwa uzinduzi huu hautakuwa na maana yoyote pasipo
mabadiliko ya kiutendaji utoaji huduma kwa wateja. Watumiaji wa huduma
zenu wanahitaji mabadiliko ya dhati ya viwango vya huduma na utendaji
ili kuwajengea imani juu ya uwezo wenu wa kuwahudumia," alisema Waziri
Mbarawa. Ofisa
Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk Kamugisha Kazaura akizungumza katika hafla ya
uzinduzi wa nembo mpya ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) pamoja na
kuzinduwa huduma ya mtandao wa kisasa wa 4G LTE leo jijini Dar es
Salaam. [/caption] Alisema Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
itafarijika zaidi itakapoona huduma za TTCL kimawasiliano zinaongoza
nchini huku zikisaidia kukua kwa sekta nyingine zinazotegemea TEHAMA
kufanikisha malengo yao. Aidha aliongeza kuwa Serikali itaendelea
kushirikiana na TTCL ili kuhakikisha inafanikiwa katika malengo yake
bila kikwazo chochote, kwani hivi sasa sekta ya Habari na Mawasiliano
inagusa shughuli nyingi za maisha ya wananchi ya kila siku, kijamii,
kiuchumi na kimaendeleo. "Hivi sasa huduma hizi sio tena jambo la ziada
katika maisha ya kila siku bali ni huduma za msingi zenye kipaumbele cha
juu katika maisha," alisema Waziri Mbarawa. Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto)
pamoja na Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Bi. Edwina Lupembe
(kulia) wakifuatilia hotuba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk Kamugisha
Kazaura (hayupo pichani)
Kwa
upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk Kamugisha Kazaura alisema
uzinduzi wa nembo mpya ya TTCL unaleta muonekano mpya wa kampuni
unaoenda sambamba na mageuzi ambayo yanaendelea katika kuboresha
miundombinu ya mtandao wa simu na data. Alisema katika safari ya mageuzi
TTCL imefanikiwa kuboresha miundombinu ya simu za mezani na mkononi kwa
kuleta teknolojia ya 2G GSM, 3G, UMTS na LTE sokoni ili kwenda sambamba
na ushindani wa soko la mawasiliano. "...Teknolojia hizi zitaisaidia
kuongeza ufanisi, ubunifu katika kutoa huduma ya simu za mezani, simu za
mkononi na huduma ya intaneti zenye ubora wa hali ya juu na ya uhakika
na gharama nafuu," alisema Dk. Kazaura. Alisema kwa sasa kampuni hiyo
inaendelea na juhudi za kuboresha miundombinu ya mawasiliano ya data
nchi nzima, hali ambayo itaongeza ubora wa huduma zetu kwa wateja wetu
wote ndani na nje ya nchi.
Post a Comment