Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

KUFUATIA ZIARA YA WAZIRI MKUU WA INDIA INAYOTARAJIWA HIVI KARIBUNI , Tunapata somo gani?


Wakati India na Tanzania zilikuwa karibu sawa mwaka 1961 wakati
Tanzania inapata uhuru, takwimu za Ushindani wa Kiuchumi Duniani za
Mwaka 2016, zimeitaja India kuwa ni taifa la kumi katika orodha ya
mataifa 10 yenye uchumi mkubwa zaidi Duniani. Mataifa tisa ya kwanza
kwa uchumi Duniani ni Marekani, China, Japani Ujerumani, Ufaransa,
Uingereza, Brazili, Italia na Urusi.


India inamiliki dollar trilioni 2.04 pato la jumla la ndani.Pato la
India likijumlishwa na mapato ya mataifa hayo tisa, yanafanya jumla ya
mapato ya ndani ya mataifa hayo kumi kuwa ni sawa na asilimia 65 ya
pato lote la dunia.



Uchumi wa India unategemea zaidi sekta ya huduma (Hospitality) kwa
asilimia 57. Tanzania inapaswa kujifunza mambo mengi kutoka India
kwasababu India imepiga hatua kubwa ya kimaendeleo katika nyanja
mbalimbali, hasa za viwanda, teknolojia, TEHAMA, kilimo, usalama na
afya.



Kinyume na fikra za sasa za Serikali ya Tanzania kuwa Sekta ya Viwanda
pekee ndiyo itakayokuza uchumi, kwa India jambo la kujifunza na
kutiliwa maanani zaidi ni jinsi nchi hiyo ilivyoweza kuijenga na
kuitegemea zaidi sekta ya Huduma (kwa asilimia 57%) kuliko sekta
zingine. Tanzania yenye vivutio vingi vya utalii kuliko India,
inayodai kuwa na Amani na Utulivu na yenye Watu Wema na Watulivu,
ilipaswa kuwa mbali zaidi katika sekta ya Huduma.



Sekta nyingine zinazochangia kukuza uchumi wa India ni Viwanda
(asilimia 26) na Kilimo kwa asilimia 17.



Serikali ya India imekuwa ikitoa misaada mbalimbali kwa Tanzania.
Misaada hiyo ni pamoja na ununuzi wa matrekta kwa ajili ya kuboresha
kilimo wenye thamani ya Dola za Marekani milioni 40 unaosimamiwa na
SUMA-JKT. Msaada mwingine ni ujenzi wa miundombinu ya maji katika
mikoa ya Pwani na Dar es Salaam uliogharimu Dola za Marekani milioni
178.125. 


 Na hivi karibuni India imekubali kusaidia ujenzi wa
miundombinu ya kusafirisha maji kutoka Ziwa Victoria hadi katika mikoa
ya Shinyanga na Tabora utakaogharimu Dola za Marekani milioni 268.35
panoja na mradi mwingine wa maji utakaogharimu Dola za Marekani
milioni 92 utakaojengwa visiwani Zanzibar


Itaendelea kesho kwa faida ya taifa

Peter Msigwa


waziri kivuli mamabo ya Nje
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top