#BreakingNews Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) limeiteua Tanzania kufanyia mkutano wake mkuu wa kila mwaka utakaoshirikisha mataifa 19, ukiongozwa na Rais wake Gianni Infatinho.
Mkutano huo mkubwa na wa kihistoria umepangwa kufanyika tarehe Februari 22 mwaka huu katika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Rais @Tanfootball Wallace Karia aliyezungumza na wanahabari hivi punde amesema mkutano huo utakuwa ajenda tofauti ikiwemo namna ya utoaji wa fedha za @FIFAcom kwaajili ya maendeleo ya mchezo wa soka.
Karia amesema ajenda nyingine ni pamoja na kuangalia changamoto za usajili wa wachezaji kwa njia mtandao (TMS), kalenda ya kimataifa ya @FIFAcom pamoja na nchi wanachama kuwa na vipaumbele vya FIFA.
Mwenyekiti wa mkutano huo ni Rais wa FIFA Giann Infatino na miongoni mwa viongozi watakaohudhuria ni katibu mkuu wa FIFA Fatma Samba Diouf Samoura.
Wengine ni sekretarieti nzima ya FIFA pamoja na rais wa shirikisho la soka barani Afrika CAF, Ahmad Ahmad na sekretariat yake nzima.
Wengine ni sekretarieti nzima ya FIFA pamoja na rais wa shirikisho la soka barani Afrika CAF, Ahmad Ahmad na sekretariat yake nzima.
Karia amesema kufanyika kwa mkutano huo nchini Tanzania ni sehemu ya kukidhi vipaumbele vyake na pia ujio huo utasaidia kuitangaza Tanzania kiutalii pamoja na kurahisisha mahusiano ya kisoka
Karia amesema sababu kubwa ya Tanzania kuteuliwa kuwa sehemu ya kufanyia mkutano huo, ni mahusiano mazuri yaliyopo kati ya viongozi wa soka la Tanzania na wale wa FIFA
Post a Comment