Rais @MagufuliJP akiwa ameshikana Mikono na kuomba dua na Mwanamuziki Nguza Vicking “Babu Seya” na wanae Johnson “Papii Kocha”, Francis na Michael walipofika Ikulu jijini leo kumshukuru kwa msamaha wake aliotoa kwao dhidi ya kifungo cha maisha walichokuwa wakitumikia.
PICHA NA IKULU
Mwanamuziki Nguza Vicking “Babu Seya” na wanae Johnson Nguza “Papii Kocha”, Francis Nguza na Michael Nguza leo wamefika Ikulu kumshukuru Rais Magufuli kwa msamaha aliotoa kwao dhidi ya kifungo cha maisha walichokuwa wakitumikia gerezani.
,,,,,,,,,,
Yaani sijui nisemaje, hapa nina furaha kubwa moyoni mwangu, nilikuwa naomba sana tangu muda mrefu nikutane nae, nimeomba sana sana, hatimaye leo nimefanikiwa na nimemwambia namshukuru sana kwa kutusamehe na sasa nipo tayari kuchapa kazi, Hapa Kazi Tu"- Babu Seya.
Post a Comment