Manchester City wanatakiwa wavunje rekodi yao wenywe ya uhamisho kwa mara ya pili ndani ya muda wa Masaa 48 kuelekea mwisho wa dirisha dogo la usajili ili kumsajili Riyad Mahrez.
Winga huyo wa Leicester mwenye uraia wa Algeria tayari amewasilisha barua ya kutaka kuondoka Klabuni hapo ili kuhamia City, ambao wamemsajili Aymeric Laporte kutoka Athletic Bilbao pauni £57millioni siku ya jana, walituma maombi ya kumsajili kwa pauni £50m lililokataliwa.
Leicester wanataka pesa mara mbili ya hizo ili wamtoe Mahrez, ambaye ana mkataba wa miaka miwili na nusu imebaki katika mkataba wa analipwa £100,000 kwa wiki. Mchezaji huyo mwenye miaka 26 anapenda kuondoka ili kuweza kushinda makombe na Man City.
Riyad Mahrez akifanya mazoezi siku ya Jumatatu -japokuwa hakufanya mazoezi na timu yake siku ya Jumanne.
Post a Comment