Kila shabiki wa soka amevutiwa na kiwango alichokionyesha "Mfalme wa Misri' kama mashabiki wa Liverpool wanavyomuita Mohamed Salah.
Winga hyuo mwenye uraia wa Misri amepata siku kwa haraka sana katika ulimwenu wa Soka kutokana na umari wake wa kutupia nyavyni magoli toka alipojiunga na kukipiga hapo Anfield.Kiwango kimekuwa kikikua kila wiki hivyo kujichukulia umaarufu kila uchao.
Liverpool walilipa kiasi cha £36.9millioni kwa Roma kuweza kupata sahihi yake kiasi kinachoonekana ni kidogo kutokana na kiwango anachokionyesha kwa sasa.Mpaka Sasa katupia magoli 28 katika mechi 34 alizocheza ambayo ni kiwango kikubwa kwa winga kufunga.
Anaelekea kuwa miongoni mwa mchezaji wa tatu wa Liverpool kuweza kufikisha katika miongo kadhaa kufikisha magoli 30 katika msimu mmoja wa EPL IWAPO ataendelea na moto huu alionao wa ktupia kambani.
Anafuata nyendo za Fernando Torres na Luis Suarez. Mashabiki wa Liverpool wanaokaa kwenye jukwaa la The Kop tayari wameshaweka nembo na bendera zenye kumtambulisha mchezaji huyu mahiri kwa sasa kutoka Bara la Afrika ambaye tayari amechaguliwa kuwa mchezaji bora Afrika.
Wakati Jurgen Klopp akichukua mikoba ya kuinoa Liverpool aliahidi kufanya kila awezalo ili wachezaji wote wenye vipaji kuweza kucheza soka na kumaliza muda wao wa soka hapo Anfield kuliko kuona vipaji kama Xabi Alonso, Javier Mascherano, Torres na Suarez.
Japokuwa,mwezi uliopita tumeona wakimuuza Philppe Coutinho kwa Barcelona hivyo kuonyesha dhamira yake bado haijatimia.Liverpool walifanya kila mbinu ili kuweza kumbakisha mchezaji huyu mzaliwa wa Brazil lakini ilibidi wamuuze kutokana na mchezaji mwenyewe kuomba kuondoka ili atimize ndoto yake ambayo ni kutua Barcelona.
Hofu imetanda kwa Wana Liverpool kuwa Salah naye anaweza kuondoka kama wengine hao nao walivyotimka
Kuna uwezekano mkubwa Mo Salah akajiunga Real Madrid baada ya mwisho wa msimu huu kuisha .Wahispania hao wanaweza kutuma maombi kwa ajili yake kama Raisi wa Chama cha Soka FA Misri Hany Abo Rida alivyosema hivi karibuni.
“Ni hakika kwa Mmisiri maarufu ulimwenguni kwenye soka lazima angependa kucheza kwenye Klabu kubwa kama Real Madrid, litakuwa jamabo jema sana kwa soka la Misri.”
Japokuwa kwa sasa ni maneno tu yanayosemwa lakini itakuwa hatasi kubwa sana iwapo matajir wa Real wataamua kumchukua ,hasa kutokana na Cristiano Ronaldo kiwango chake kuwa kwenye mashaka kutokana na umri kuwa mkubwa na presha kubwa aliyonayoo sasa Kocha Zinedine Zidane, wanatakiwa kweli kusajili mchezaji mwenye kipaji Kikubwa.
Je Liverpool wanatakiwa Kuogopa ?
Na watafanyaje kuhakikisha Salah anabaki kwa kipindi kirefu ?
Kwanza, Klopp kwa sasa hana shaka kwa ukweli kwamba Salah ni mmwenye furaha na kuridhika kuwa Anfield. Kweli,winga huyo amekuwa na mafanikiwa ndani ya uwanja kwa kipindi cha miezi saba aliyoishi ndani ya Liverpool nao kuwa mtu mzuri kwao.
Klopp amemsaidia kunyanyua kiwango chake katika levo nyingine kwa kumpa ujuzi katika maamuzi anayofanya uwanjani kuwa ni wakati gani na eneo gani afanye nini.
Salah sio Msouth Amerika.Ambao wana ndoto za kucheza Uhispania toka udogoni kama kina Suarez au Coutinho.
Amekuwa akiongozwa na wakala wake Ramy Abbas Issa, aliyechukua mikoba ya wakala aliyesimamia uhamisho wake kutoka Basel kwenda Chelsea 2014.
Salah amesaini kandarasi ya miaka mitano kwa mshahara wa £90,000 kwa wiki mwanzoni mwa msimu huu na unampa nafasi ya kuongeza zaidi muda na bonasi mbalimbali uhamisho ambao ulikuwa makini kwake ukizingatia mwaka huu wa Kombe la Dunia.Anastahili kuwa karibu na Virgil van Dijk kuwa miongoni mwa wachezaji wanaolipwa zaidi.
Coutinho aliondoka baada ya miezi 12 toka alipoongeza au kusaini mkataba mpya japokuwa haukuwa na kipingele chenye kuonyesha kiasi cha fedha ambacho klabu yenye kumtaka ingetakiwa kulipa kwanza lakini Liverpool waliweza kutaka kiwango kikubwa cha fedha na Barcelona wakakubali kulipa.
Liverpool hawatakubali kufanya makosa hayo kwa Salah msimu huu.
Wakati vuguvugu la kuhama likishika kasi kutokana na kiwango chake kupanda,maneno kama kiwango chake kina thamani ya £200million sio uwongo, lakini Klopp anasema hana bei.
Salah amekuwa na mwanzo mzuri msimu huu na Liverpool wameonyesha kumpa kila msaada ili aweze kutimiza ndoto na matumaini yake.Hivyo kuweza kuapata nafasi ya Mabingwa wa Ulaya (UEFA) itakuwa jmabo zuri sana kwake.
Mfalme wa Misri ni turufu nzuri sana kwa Liverpool na wanatakiwa wafanye kila mbinu kuhakikisha wanakaa vizuri na Mfalme huyu Mo Salah.
Na Chediel Charles
Kwa Msaada wa Majarida ya mitandaoni.
Post a Comment