Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

MAN CITY YAONDOLEWA KOMBE LA FA NA WIGAN ATHLETIC

Hapo Usiku Wigan Athletic ilisitisha matumaini ya ManCity ya kupata mataji mengi baada ya kuwashangaza katika mechi ya raundi ya tano ya kombe la FA.
Klabu hiyo ya ligi ya daraja la kwanza nchini Uingereza ilistahimili presha ya mara kwa mara kutoka kwa viongozi hao wa ligi ya EPL na kutumia fursa ya kadi nyekundu aliyopewa Fabian Delph wakati Will Grigg alipofunga katika dakika 11 kabla ya kukamilika kwa mechi hiyo.
Shambulizi hilo la kimo cha nyoka lilizua vioja katika uwanja wa DW stadium huku kiungo wa kati wa City Fernandinho akikosa nafasi ya wazi muda mfupi baada ya Delph kupewa kadi nyekundu kwa kumchezea visivyo Max Power.
Kisa hicho kiliwafanya makocha wote wa pande zote mbili kurushiana maneno wakati wa muda wa mapumziko.
Na kulikuwa na vioja zaidi baada ya mechi hiyo kukamilika huku mshambuliaji Sergio Aguero akihusishwa na mzozo na mmoja wa mashabiki waliovamia uwanja huo.

City waliwashambulia wenyeji wao baada ya bao hilo la Grigg ambalo lilikuwa shambulio kutoka maguu 20 huku kichwa cha Danilo kikidakwa na kipa Christian Walton katika dakika za lala salama.
Na mpira ulipokamilika kulikuwa na shangwe na nderemo ndani ya uwanja kutoka kwa mashabiki wa nyumbani.
Kwa upande mwengine mashabiki wa City walikuwa wamekasirika na vitu vilirushwa ndani ya uwanja baada ya wachezaji kuondoka.

Lakini hilo halikuaribu usiku wa Wigan walioishinda City katika kombe hilo kwa mara ya tatu ndani ya misimu sita.
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top