Klabu ya Simba imefanikiwa kufuzu hatua inayofuata ya michuano ya Caf Confederation Cup kwa jumla ya magoli 5-0 baada ya ushindi wao goli 1-0 ugenini dhidi ya Gendarmerie ya Djibouti.
Simba walifanikiwa kupata goli pekee lililofungwa na mshambuliaji mganda Emanuel Okwi dakika ya 53 kwenye uwanja wa Stade de Vile jijini Djibouti.
Mchezo wa kwanza uliochezwa Februari 11, 2018 kwenye uwanja wa Taifa Simba ilishinda 4-0 hivyo ushindi wa goli 1-0 ugenini unaipa nafasi ya kusonga mbele kwa magoli 5-0 baada ya michezo miwili.
Baada ya kuiondosha Gendarmerie kwenye mashindano, Simba itakutana na Al Masry ya Misri katika hatua inayofuata.
Al Masry imeitoa Green Buffalos ya Zambia kwa jumla ya magoli 5-2. Al Masry walishinda 4-0 kwenye mchezo wa kwanza wakiwa nyumbani (Misri) lakini leo wamechezea kichapo cha mabao 2-1 ugenini (Zambia) lakini wamesonga mbele kwa wastani mzuri wa magoli.
Post a Comment