Lionel Messi amefunga goli lake la kwanza katika dhidi ya Chelsea katika michezo tisa ns dakika 730 ambayo Klabu hizo zimekutana uwanjani. Na ukiwa ni mkwaju wake wa 30 kupiga dhidi ya Chelsea.
Pamoja na kuwa na mabao 595 aliyofunga lakini hakuwahi kufunga goli lolote hapo kabla.
Lakini usiku wa leo Lionel Messi amefuta mkosi huo baada ya kufunga bao lake la kwanza dhidi ya Chelsea japo bao lake lilikuwa la kusawazisha baada ya Chelsea kutangulia kupitia Willian.
Bao la leo la Willian lilikuwa bao lake la 9 katika klabu bingwa Ulaya(muda wote) na sasa anakuwa amefunga mabao 6 kati ya hayo nje ya box huku Messi sasa anakuwa na jumla ya mabao 18 vs timu za Uingereza.
Bao la willian alifunga dakika ya 62 kabla ya Messi kusawazisha dakika 75 ya mchezo.
Post a Comment