Mlinzi wa Colombia ,Yerry Mina anakaribia kujiunga na Klabu ya Everton ambao wamefikia makubaliano na Barcelona kumsaini, kwa pauni milioni 28.5 kwa mkataba wa miaka mitano.
Wakati huo huo Everton wamewaambia Manchester United kuwa watamchukua beki ya miaka 28 raia wa England Chris Smalling au mlizni wa Sweden Victor Lindelof, 24, ikiwa klabu hizo mbili hazitaafikia makubaliano kuhusu mlinzi raia wa Argentina Marcos Rojo, 28
Manchester United wanajiandaa kutoa ofa kwa beki wa Leicester Harry Maguire, 25, na kwamba sasa wanaweza kulipa pesa nyingi zaidi katika rekodi kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa England.
Wakati huo huo Manchester United wamefanya mawasiliano na Bayern Munich kumsaini mlinzi mwenye miaka 29 mjerumani Jorome Boateng kwa kima cha pauni milioni 44.5.
Chelsea wako katika nafasi nzuri kumsaini kwa pauni milioni 75 wing'a wa Crystal Palace na Ivory Coast Wilfried Zaha, 25, baada ya Tottenham kujiondoa
Ofa ya Leicester ya pauni milioni 10 imekataliwa kwa mlinzi wa Brentford Chris Mepham, 20, huku nao Bournemouth wakimmezea mate mchezaji huyo wa kimataifa wa Wales
Wolves wanataka kuilipa Middlesbrough pauni milioni 22 kwa awamu kwa wing'a raia wa Uhispania Adama Traore, 22, badala ya malipo yote kwa jumla kwa kulipa kwanza paunia milioni 18.
Crystal Palace wako kwenye mazungumzo kumsaini mshambuliaji wa Red Bull Salzburg raia wa Israel Munas Dabbur, 26
Mshambuliaji wa Uhispania Lucas Perez, 29, anataka kusalia Arsenal na kupigania nafasi yake katika timu licha na klabu ya Ureno ya Sporting Lisbon kuonyesha dalili ya kumsaini.
West Ham wamekamilisha mbio za kumwinda wing'a wa Porto Yacine Brahimi, 28, baada ya kushindwa kukubaliana na mchezaji huyo wa kimataifa wa Algeria.
West Ham wametoa ofa ya pauni milioni 10 kwa mchezaji wa Le Havre mwenye miaka 20 raia wa Ufaransa Harold Moukoudi.
CHANZO:Vyombo vya habari Kimataifa.
Post a Comment