Manchester United itakabiliwa na 'wakati mgumu' iwapo haitaongeza mchezaji yeyote katika dirisha la usajili linalokaribia kufungwa Alhamisi Kocha Jose Mourinho.
Mashetani wekundu hao wamemaliza msimu wa maandalizi kwa kipigo cha goli 1-0 dhidi ya mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich jana Jumapili.
Javi Martinez alifunga kwa kichwa cha kuparaza kipindi cha pili na kuwapa ushindi huo Bayern mechi iliyotawaliwa na mabingwa hao.
"Bosi wangu anajua ninachohitaji na imebaki siku chache ,nitasubiri na kuona kama tutaongeza mchezaji ," Mourinho alikiambia kituo cha MUTV.
"Vilabu vingine tunaoshindana nao wanatimu nzuri na imara sana. au wameimarisha kikosi vizuri sana kama Liverpool, ambao wamenunua kila kitu na kila mchezaji.
"Tusipoimarisha timu yetu vizuri huu utakuwa msimu mbaya sana kwetu."
United wameshasajili wachezaji watatu mpaka sasa - Kiungo MBrazil Fred kwa £47m, Mlinzi wa Kireno Diogo Dalot na golikipa chaguo la tatu Lee Grant.
Manchester United wanataraji kufungua pazia la EPL na Leicester City Uwanja Old Trafford siku ya Ijumaa.
Post a Comment