Manchester City, Manchester United, Tottenham na Liverpool leo zitajua timu watakazo kabiliana nazo katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya katika hatua ya makundi yatakayopangwa leo jioni Alhamisi.
Makundi hayo yatapangwa leo Alhamisi katika mji wa Monaco.
Kumepangwa kuwa na makapu manne yenye timu nane, ambapo kila timu kutoka kila kapu itaunda Kundi,lakini kwa timu zinazotoka nchi moja haziwezi kuwa kundi moja.
Mabingwa wa EPL Man City,waliotolewa na Liverpool katika hatua ya robo fainali msimu uliopita, wako kapu la kwanza na mabingwa watetezi Real Madrid, Mabingwa wa Europa Ligi Atletico Madrid, Barcelona, Bayern Munich, Juventus, Paris Saint-Germain na Lokomotiv Moscow.
Man United na Spurs, waliotolewa kwenye hatua ya 16 bora msimu wa 2017/2018,wako kapu la pili,lenye timu za Borussia Dortmund, Porto, Shakhtar Donetsk, Benfica, Napoli na Roma.
Kikosi cha Jurgen Klopp’s Liverpool watakuwa kapu la tatu na Schalke, Lyon, Monaco, Ajax, CSKA Moscow, Valencia na PSV Eindhoven.
Mabingwa nchini Serbian Red Star, bingwa 1991, atakuwa Viktoria Plzen, Club Brugge, Galatasaray, Young Boys, Inter Milan, Hoffenheim na AEK Athens.
Mechi za mwanzo za makundi zitaanza kati ya Septemba 18 na 19, huku fainali itapigwa katika uwanja wa nyumban wa Atletico Madrid’s Wanda Metropolitano Stadium mnamo June 1.
Na Chediel Charles
CHANZO:Vyombo vya habari vya kaimtaifa.
Post a Comment