Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

JK AANDALIWA MAPOKEZI MAKUBWA BAGAMOYO

Na Richard Mwaikenda, Dodoma
MWENYEKITI mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Jakaya Kikwete ameandaliwa mapokezi makubwa na wanaCCM wilayani Bagamoyo kesho baada ya kung'atuka wadhifa huo, kwenye Mkutano Mkuu Maalum Dodoma.

Akielezea kuhusu mapokezi hayo mjini Dodoma jana, Katibu Mwenezi wa CCM, Wilaya ya Bagamoyo,Kassim Gogo alisema kuwa mapokezi hayo yataanzia Chalinze hadi Bagamoyo.

Alisema kuwa wanaCCM wa wilaya hiyo wanajisikia furaha sana kuona Jakaya Kikwete ambaye ni mzaliwa wa Kijiji cha Msoga, wilayani humo, ameng'atuka salama baada ya kukitumia chama na serikali kwa miaka kumi.

Alisema kuwa jambo lingine linalowapa faraja ya kuandaa mapokezi hayo ni kwamba Jakaya Kikwete ameng'atuka uongozi kwa kukiacha chama salama na nchi ikiwa salama pia.

Gogo, alisema kuwa katika mapokezi hayo watakuwepo madiwani wote wa wilaya hiyo, viongozi wa CCM, wabunge wote wa Mkoa wa Pwani na wananchi. 

Alisema kuwa wakati wa hafla hiyo pia Mwenyekiti mstaafu, Kikwete atakabidhiwa zawadi mbalimbali ikiwemo kumvisha gwanda ili awe mlezi wa CCM Mkoa wa Pwani.

Katika sherehe za mapokezi zitakazofanyika mbele ya Makao Makuu ya Ofisi za CCM za wilaya hiyo zilizopo Bagamoyo Mjini, patakuwepo ngoma za asili ya makabila ya Wakwere, Wazaramo na Wazigua pamoja na wasanii mbalimbali pia watatumbuiza.

Alisema kuwa Kikwete akiwa amepumzika baada ya kung'atuka, watapata wasaa wa kuchota hekima na burasa zake ya jinsi ya kukiongoza chama hicho na serikali pia.

KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM JANA MJINI DODOMA



Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete(kulia) akifuatana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli kabla ya kuingia katika ukumbi kikao cha siku moja cha Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM kilichofanyika leo Ikulu ya  Chamwino Mkoani Dodoma,[Picha na Ikulu.]
Baadhi ya Wajumbe wa Kikao cha Kamati Kuu ya CCM wakiwa katika Ukumbi wa Mkutano uliofanyika leo chini ya Mwenyekiti wake Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma,[Picha na Ikulu.] 
Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Nd,Majaliwa Kassim Majaliwa wakati wa Mkutano wa siku moja wa Kamati Kuu ya CCM uliofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu  Chamwino Mkoani Dodoma na kuongozwa na Mwenyekiti wake Rais Msataafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, [Picha na Ikulu.] 

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiendesha Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa kilichofanyika Mkoani Dodoma. Kulia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na kushoto ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein wakifurahia jambo kabla ya kuanza kwa kikao cha cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa kilichofanyika Mkoani Dodoma.

SIASA NA KAZI

Mfanyabiashara katika soko la Pasua, akimsikiliza kwa makini Msemaji Mkuu wa CCM, Ole Sendeka wakati wa mkutano wa hadahara uliofanyika eneo la Bomambuzi, mjini Moshi mkoani Kilimanajaro .

SENDEKA: LOWASSA ANADANGANYA WATANZANIA KUTAFUTA MASLAHI KISIASA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Aliyekuwa mgombea Urais wa UKAWA kupitia CHADEMA, Ndugu Edward Lowassa, Aprili 7, 2016 alifanya mazungumzo na Wanazuoni kutoka katika vyuo vikuu vya ndani na nje ya nchi.
Katika mazungumzo hayo, Ndugu Lowasa aligusia masuala mbalimbali ya Kitaifa yakiwemo hali ya siasa nchini, kuachisha kazi watumishi wenye tuhuma mbalimbali, na kile alichokiita tatizo la mfumo nchini.
Alichokifanya Ndugu Lowassa ni kutaka kuwaaminisha Watanzania masuala yasiyo sahihi kwa maslahi ya kisiasa, kwani ukweli ni kwamba; Mosi, Rais John Pombe Magufuli hatafuti umaarufu, badala yake yeye na Serikali yake wanachapa kazi ili kuwaletea maendeleo Watanzania kwa ujumla.
Pili, kuhusu suala la mfumo, Tanzania haina tatizo la kimfumo, kwani iliyopo, iliyowekwa tangu awali na waasisi wa Taifa letu, Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Abeid Aman Karume ni imara na imekuwa ikiboreshwa kulingana na mahitaji.
Ifahamike hakuna mahali popote duniani ambako mfumo wa nchi unajiendesha wenyewe, siku zote mfumo huongozwa na kuendeshwa na binadamu ambao kwa udhaifu wa ama kibinadamu au wa kukusudia, hufanya makosa yanayohitaji kusahihishwa kwa taratibu zilizowekwa.
Tatu, Hakuna mtumishi aliyeachishwa au kusimamishwa kazi kwa sababu ya hali ngumu ya uendeshaji wa Shirika lolote, isipokuwa hatua hiyo imechukuliwa ili  kupisha uchunguzi kutokana na tuhuma mbalimbali za ukiukaji na matumizi mabaya ya ofisi na madaraka, ubadhirifu, uhujumu uchumi na ufisadi.
 
Chama Cha Mapinduzi kina ushahidi wa utendaji wa Ndugu Lowasa akiwa Waziri Mkuu namna alivyoendesha zoezi la kusimamisha na kufukuza kazi na kuwadhalilisha watumishi bila kufuata taratibu, hali hiyo ni tafauti sana na hii ya sasa, kwani kila anayesimamishwa kazi, anasimamishwa kwa kufuata taratibu zote, ili kuhakikisha kila mtumishi anatendewa haki ya kusikilizwa.
Na katika hili la kuwasimamisha kazi watumishi wa umma wanaotuhumiwa kwa ufisadi, wizi na matumizi mabaya ya ofisi, Chama Cha Mapinduzi kitaendelea kuunga mkono, kutokana na baadhi yao kuwa chanzo cha  shughuli za maendeleo nchini.
Kiongozi au mwanasiasa anayemkosoa Rais Magufuli katika hatua anazozichukua hivi sasa, ikiwa ni pamoja na kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma, ni wa kutiliwa shaka kwani kufanya hivyo ni sawa na kutetea wizi, ufisadi na uporaji wa rasilimali za nchi. 
Ndugu Christopher Ole Sendeka   
MSEMAJI WA CCM 
MJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
                                                     08/04/2016       

KAMATI KUU YA CCM YATEUA WAGOMBEA WA KUJAZA NAFASI MBALI MBALI ZILIZO ACHWA WAZI



Katibu wa Itikadi na Uenezi Mhe. Nape Nnauye akiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa NEC, Makao Makuu ya CCM, Ofisi Ndogo Lumumba.


Jana tarehe 07/02/2016 Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ilikuwa na kikao maalum cha siku moja mjini Dodoma. Kikao hicho kiliongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa CCM Dr. Jakaya Mrisho Kikwete. Kikao hicho kilikuwa na kazi ya kuteua wagombea wa nafasi mbalimbali zilizo wazi za uongozi ndani ya CCM mikoani na wilayani ambazo uteuzi wake upo kwenye Mamlaka ya Vikao vya Chama Taifa.

JK AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU MAALUM YA CCM MKOANI DODOMA

 Mjumba wa Kamati Kuu ya CCM, Rais Dk. John Magufuli akimkaribisha, Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete alipowasili, Ikuu Ndogo ya Chamwino mkoani Dodoma, kuendesha Kikao Cha Kamati Kuu Maalum ya CCM
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete akiwa na Mjumba wa Kamati Kuu ya CCM, Rais Dk. John Magufuli alipowasili, Ikuu Ndogo ya Chamwino mkoani Dodoma, kuendesha Kikao Cha Kamati Kuu Maalum ya CCM
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akimsalimia Mjumbe wa Kamati Kuu, Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan baada ya kuwasili ukumbini kuendesha kikao cha Kamati Kuu ya CCM leo, Chamwino mkoani Dodoma. Kulia ni Rais Magufuli
  Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akimsalimia Mjumbe wa Kamati Kuu, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idi, baada ya kuwasili ukumbini kuendesha kikao cha Kamati Kuu ya CCM leo, Chamwino mkoani Dodoma
  Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akimsalimia Mjumbe wa Kamati Kuu, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula, baada ya kuwasili ukumbini kuendesha kikao cha Kamati Kuu ya CCM leo, Chamwino mkoani Dodoma
  Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akimsalimia Mumbe wa Kamati Kuu, Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa,  baada ya kuwasili ukumbini kuendesha kikao cha Kamati Kuu ya CCM leo, Chamwino mkoani Dodoma
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Rais Dk. John Magufuli akimsalimia Mjumbe wa Kamati Kuu mwenzake, Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Maaliwa
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimsalimia Mumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Rais Dk. John Magufuli kabla ya kikao kuanza. Katikati yao ni Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete
 Viongozi hao wakiendelea na mazungumzo ya hapa na pale kabla ya kikao kuanza
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu akaya Kikwete akifurahia ambo na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Rais Dk. John Magufuli na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kabla ya kikao kuanza 
 Wajumbe wakisimama ukumbini kumlaki Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete kabla ya kikao kuanza
 Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Rais Dk John Magufuli na Makamu wake, Mama Samia Suluhu Hassan wakiwa ukumbini
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye akibadilishana mawazo na Katibu wa NEC anayeshughulikia mambo ya Nje Dk. Asha-Rose Migiro ukumbini. Kulia ni Katibu wa NEC Oganaizesheni Mohammed Seif Khatib
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rajabu Luhavi akiwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ally Vuai na Balozi Seif Ali Idd  ukumbini
 Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Pindi Chana na Asha Aboud wakibadilishana mawazo ukumbini 
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitoa utangulizi kumkaribisha Mwenyekiti kufungua kikao
Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiendesha kikao cha Kamati Kuu Maalum ya CCM, leo, Ikulu Ndogo ya Chamwino mkoani Dodoma. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

KUELEKEA MKUTANO WA BUNGE CCM WAKUTANA DODOMA KUWEKA MIKAKATI YA KUWAKABILI UKAWA

Wabunge wa CCM wakimsikiliza Mbunge wa Kibakwi Mhe. Boniface Simbachawene wakati akifafanua mambo mbali mbali kwenye ukumbi wa NEC, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma.
Mbunge wa Jimbo la Isimani Mhe. William Lukuvi akichangia hoja kwenye semina ya wabunge wa CCM.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (katikati) ambaye ndie mwenyekiti wa kikao maalum chenye kutoa semina elekezi kwa wabunge wa CCM, kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Mhe. Philip Mangula na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (kushoto).
Mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi Mhe. Mwigulu Nchemba akifuatilia kwa makini hoja mbali mbali zilizotolewa na wabunge wa CCM kwenye semina maalum elekezi kwa ajili ya wabunge wa CCM mjini Dodoma.

KAMATI KUU(CC) YA CCM YAMPONGEZA RAIS MAGUFULI


Mwenyekiti wa CCM na Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho kikwete akiongozana na Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli , Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Mhe Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahmana Kinana kabla ya kuanza kwa Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa jijini Dar es salaam leo Desemba 7, 2015.


Mwenyekiti wa CCM na Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho kikwete akiongoza Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa jijini Dar es salaam leo Desemba 7, 2015.


Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipigiwa saluti na Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahmana Kinana kabla ya kuanza kwa Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa jijini Dar es salaam leo Desemba 7, 2015.


Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu Dkt Salim Ahmed Salim. wengine ni Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa, Makamu wa Rais Mhe samia Suluhu Hassan na Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahmana Kinana kabla ya kuanza kwa Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa jijini Dar es salaam leo Desemba 7, 2015. 

 Kamati Kuu ya CCM (CC) iliyoketi leo hii chini ya Mwenyekiti Jakaya Kikwete imempongeza Rais Magufuli kwa mapambano aliyoyaanzisha na kumtia moyo kuwa CCM,kwa ujumla wake,iko pamoja naye.
Lakini,CC imemshauri na kumtaka Rais Magufuli kujiridhisha vya kutosha kabla ya kutumbua majipu mbalimbali ya kitaifa. Imesemwa kuwa nchi yaweza kuendeshwa kwa majungu na hivyo wananchi kuishi kwa visasi na kuchongeana. Ni kama CC imemfunga Speed Governor Rais Magufuli 'kimtindo'.

Pia,CC imemtaka kuwa makini na teuzi zake za sasa na zijazo. Imedhihirika leo kuwa Rais Magufuli alikuwa akisubiri kikao cha CC ili kuteua na kutangaza Mawaziri. Sasa mambo yatafanyika!

COSATO CHUMI AMALIZA TATIZO LA VITANDA HOSPITAL YA MAFINGA MJINI


Pichani Mbunge wa jimbo la Mafinga mji ni Cotato chumi akimkabidhi msaada wa  vitanda ,magodoro pamoja na vifaa mbalimbali  kaimu mganga mkuu wa hospitali ya Mafinga dk Abdul Msuya juzi 
 baadhi ya waandishi wa habari wakifuatiliwa ugawaji wa vifaa hivyo wakati wa makabidhiano
 Mbunge wa Mafinga mjini Cosato Chumi akikabidhi vifaa hivyo kwa vitendo
Baadhi ya wadau na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi CCM walihudhulia tukio hilo 
............................

TATIZO la upungufu wa vitanda katika wodi ya akina mama na watoto katika hospitali ya wilaya ya Mufindi mkoani Iringa ambalo kwa muda mrefu limekuwa chanzo cha msongamano na uwalazimu baadhi ya wagonjwa kulala sakafuni sasa limepatiwa ufumbuzi baada ya uongozi wa hospitali hiyo kupokea msaada wa vitanda na vifaa tiba kutoka kwa mdau wa maendeleo katika sekta ya afya.

mbunge wa Mafinga Mjini (CCM) Cosato Chumi alisema kuwa kwa muda mrefu hospitali hiyo ilikuwa ina upungufu wa vifaa mbalimbali ikiwemo vitanda hali iliyofanya kuandika maandiko mbalimbali kwa wahisani  wa nje ya nchi ili kuweza kumsaidia kupata vifaa hivyo .
  
Alisema kuwa umefika wakati sasa wadau mbalimbali, mifuko ya kijamii na makampuni kujenga utamaduni wa kusaidia watu wenye mahitaji mbalimbali wakiwemo watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu na wagonjwa hospitalini kwani kufanya hivyo ni sehemu ya kurudisha kile wanachokitapa kwa jamii.

“Unajua afya ni kila kitu katika maisha ya binadamu hivyo lazima nitekeleze ahadi zangu nilizotoa wakati wa kampeni na wanachi lazima tufanye kazi kwa kujituma ili tumuunge mkono rais wetu ambaye anania ya ya kutuletea maendeleo na kuwataka wadau mbalimbali kusaidia jamii zenye mahitaji na kuacha kutegemea serikali pekee “ alisema
Chumi aliwaomba wananchi wa jimbo hilo kuunga mkono kwa kufanya kazi kwa nguvu zote ili walete maendeleo kwa pamoja maana akifanya kazi pekee yake bila wao hawezi kuleta maendeleo pekee yake.
  
Msaada huo wa vitanda 16 na magodoro 11 na vitu mbalimbali umetolewa na taasisi binafsi inayojishughulisha na masuala ya afya ya nchini Astralia ijulikanayo kama “Rafiki Surgical Mission” kwa uratibu wa ofisi ya mbunge wa jimbo la Mafinga mjini 

Alisema kuwa msaada huo aliopatiwa  na rafiki zao hawajatoa hata senti tano bali huwa marafiki hao wanachangishana fedha na kununua vifaa hivyo na kisha kuvisafirisha mpaka bandari kavu ambapo hapo ndio hutumia garama kusafirisha vifaa hivyo mpaka sehemu husika

“Ndugu zangu nadhani kila mmoja alikuwa akifahamu machungu waliyokuwa wakipata mama zetu wanapokuja kujifungua kwa kukosa sehemu za kujifungulia lakini leo hii msaada huu utatusaidia sana na yoyote atakayeguswa na anaweza kuja na kuchangia chochote maana mufindi ni yetu sote na mufindi itajegwa na wanamufindi wenyewe”alisema

Alisema jambo kubwa lilokuwa likimuumiza kicha kila kukicha ni tatizo la vifaa katika hospital, elimu  pamoja na tatizo la maji hivyo ni wakati wawanamafinga kushikana kwa pamoja katika kusumkuma mbele gurudumu la maendeleo ili kuendana na kauli mbiu ya sasa ya HAPA NI KAZI TU.

Akipokea msaada huo kaimu mganga mkuu wa hospitali ya Mafinga dk Abdul Msuya alisema kuwa msaada wa vitanda hivyo na magodoro na  vifaa mbalimbali utakuwa umemaliza kabisa tatizo la vitanda hospitalini hapo licha ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo zinaweza kumalizika endapo kutatokea mdau mwingine kuwasaidi Kwa upande wake katibu wa ccm wilaya ya Mufindi Jimsoni Muhagama
alimpongeza mbunge huyo kwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo huku akimwambia kuwa ni wakati wa kutekeleza kazi kwa vitendo na wala si maneno kwani wananchi wanapaswa kutatuliwa kero mbalimbali zinazowakabili badala ya kupiga porojo zisizo na msingi .

Mhagama alisema kuwa kila mmoja anapaswa kuwajibika ipasavyo katika nafasi yake kwani kasi anayokwenda nayo Rais John Magufuli si ya mchezo bali ni ya mchaka mchaka na ili nchi iweze kusimama katika mstari ulionyoka kila mmoja anapaswa kucheza wimbo wa mchaka mchaka

‘’Huuu si wakati lelemama huu sio wakati mchezo mchezo ni wakati wa uwajibikaji ,hakika Tanzania tumepata kiongozi mchapa kazi tazama sasa ni siku ya 27 nchi inaongozwa na watu wanne lakini kila sektaa imenyoka na mimi  nasemaa Magufuli wanyooshe tu kwa kuwa watu walikuwa wakifanya kazi kwa mazoeya bila ya kuangalia madhara wanayopata
watanzania swengi

Hata hivyo Mhgama alisema kuwa kwa kuwa kipindi cha muda mchache nchi inaongozwa na watu wachache na nchi imesimama haoni sababu ya kuwa na baraza kubwa la mawaziri bali Rais Magufuli achague baraza dogo kama
la watu 10 ili kupunguza mzigo kwa serekali yake ya kuwa na mawziri wengi wasiokuwa na tija  .

NAPE ASEMA CCM ITAMPA USHIRIKIANO MKUBWA DK. MAGUFULI ASIMAMIE ILANI VIZURI

Mhariri Mtendaji wa New Habari Corporation Ltd, Absalom Kibanda akimkarbisha Karibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye ambaye pia ni Mbunge wa Mtama, alipotembelea Ofisi za kampini hiyo leo, Sinza jijini Dar es Salaam
 Karibu sana
 Karibu sana hapa ni ofisini kwako
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana na Mhariri wa Habari wa gazeti la Mtanzania, Bakari Kimwanga
 Mkurugenzi wa Mawasiliano wa CCM, Godfrey Chongolo akisalimiana na Kibanda
 Wakienda ukumbini

 Wakiwa katika mazungumzo
 Kimwanga akinukuu dondoo za mazungumzo
 Khamis Mkotya akiuliza swali
 Nape akijibu swali
 Mazungumzo yakiendelea
 Asha Bani akiandika dondoo za mazungumzo
 Nape na Hussein Bashe wakifurahia jambo katika mazungumzo
 Naam hayo ndivyo yalivyo.....
 Mkurugenzi wa New Habari Corporation  Erasto Matasya akizungumza






 Mazungumzo baada ya mazungumzo
Nape akiwa na Absalom Kibanda na Asha Muhajj
 Nape akiwa na Asha Bani

Nape akiagana na Bashe kabla ya kuondoka. Picha zote na Bashir Nkoromo
HABARI KAMILI NA BASHIR NKOROMO
.....
Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimesema, kitampa ushirikiano mkubwa, Rais Dk. John Magufuli, ili aweze kwa ufanisi zaidi mapambano yake dhidi ya mafisadi na mikakati mingine ya kuinua uchumi wa Watanzania.

Kimesema, kitampa ushirikiano huo Rais Dk. Magufuli, kwa sababu, aliyoanza kuyafanya na atakayoyafanya baadaye katika uongozi wake wa Urais anatekeleza yale yaliyomo katika ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2015-2020.

Hayo yalisemwa na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alipokuwa akijibu maswali kadhaa yaliyoulizwa na baadhi ya wahariri, aliokuwa akizungumza nao, katika ziara aliyofanya leo, katika Kampuni ya New Habari Corporation, Sinza jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wahariri, waliohoji ni kwa nini CCM haijitokezi kumpongeza Dk. Magufuli katika juhudi ambazo ameanza kuonyesha katika kupambana na ufisadi ikiwemo kubana fedha za walipa kodi ambazo zingepotea bure katika masuala yasiyo ya lazima na wakati huohuo kuanza kuwabana wafanyabiashara wanaodaiwa kukwepa kulipa ushuru.

"Yapo mengi tuliyoanisha katika ilani yetu ya Uchaguzi, na yote yahahusiana sana na haya mnayoyaona yanafanywa na Rais Dk. John Magufuli, tena Ilani hii tumeitunga hata kabla ya kumteua kugombea Urais, Sasa anachofaya ni kuitekeleza ilani hii, isipokuwa mbinu anazotumia ni ubunifu wake na hili hatuna tatizo nalo kama Chama maana kiongozi wa aina hii ndiye tuliyemtaka", alisema Nape.

"Najua wapo wanaojaribu kutengeneza magingira ya kumtaka kumtenganisha Dk. Magufuli na CCM, nawambieni Dk. Magufuli ni zao la CCM na mwana CCM Kindakindaki, hivyo ni upotoshaji wa hali ya juu kujaribu kuuaminisha umma kwamba anayofanya Dk. Magufuli hayana uhusiano na maelekezo ya CCM", aliongeza Nape.

Alisema, baada ya kutengeneza ilani yake, CCM, ilidhamiria kwamba, awamu hii ya tano ni ya kutafsiri uchumi katika nyanja za huduma za Jamii, ikiwemo miundomboni, maji, afya na elimu.

"Ni kutokana na lengo hili, ndiyo sababu tukakaa kwa makini na kuhakikisha ilani hii ya sasa tunamkabidhi mwana CCM ambaye utekelezaji wake hautakuwa wa mashaka mashaka, Ndiyo huyo Dk. Magufuli, bila shaka sasa na ninyi ni mashahidi mmeanza kuuona utekelezaji wake wa ilani", alisema Nape.

Akizungumzia kuhusu Rais Dk. Magufuli kuchelewa kutangaza Baraza lake la Mawaziri, Nape alisema, Chama Cha Mapinduzi kimeshaunda serikali kwa kumpata Rais, kilichobaki sasa ni kwa Rais mwenyewe kuteua watendaji wake, lakini katika kufanya hivyo hakuna mda aliopangiwa kuanza kufanya hivyo na hashurutishwi na Chama wala sheria.

Nape alisema, Dk. Magufuli hachelewi kuteua Baraza la Mawaziri kwa sababu anakosa wakuwateua, isipokuwa, anayo namna na mda ambao mwenyewe Kama Rais amejipangia, na mda huo ukijiri wa kuamua kufanya hvyo atafanya.

"Tatizo hapa ni kwamba mnayo kiu kubwa ya kutaka kujua nani atawateua, sasa kiu yenu imepita kiasi, ndiyo maana mnaanza kuhoji, lakini mimi naamini Dk. Rais Magufuli ataikata kiu yetu, wala msipate taabu ya kuhoji kila kukicha", alisema Nape.

Nape alisema, mbali na Chama kutengeneza ilani ambayo italeta mageuzi makubwa ya kiuchumi hapa nchini, pia Watanzania watarajie kuona mageuzi makubwa ndani ya CCM, kwa sababu yapo njiani kuwadia.

"Kama ilivyo kawaida yetu, kila baada ya uchaguzi mkuu huwa tunafanya tathmini, baada ya tathmini hiyo, huwa lazima tufanye mageuzi kwa yale ambayo tumebaini kuwa ni kikwazo kwa uhai na maendeleo ya Chama katika nyanja mbalimbali, na mageuzi haya tunayafanya kuzingatia mahitaji ya sasa na wakati ujao", alisema Nape.

Kuhusu Mwenyekiti wa sasa Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete kumwachia Ueneyekiti Rais Dk. Magufuli, Nape alisema, hayo si mambo mageni kwa CCM, imekuwa ikifanyika katika awamu zote za Urais, hivyo Kikwete anaweza akaamua kumwachia kabla ya uchaguzi mkuu wa CCM utakaofanyika mwaka 2017 au kabla ya hapo akiona inafaa.

Zanzibar
Akizungumzia mgogoro wa Zanzibar uliotokana na kufutwa uchaguzi mkuu wa Rais wa Zanzibar, Nape alikiri kamba ni mbaya na unaitia doa Tanzania, akisema, lakini akasisitiza kwamba njia pekee ya kuumaliza ni kwa mazungumza baina ya viongozi wa ndani bila kushirikishwa mataifa ya nje.

Alisema, msingi wa mgogoro uliojitokeza Zanzibar, si wa kisheria, bali ni wa kisiasa zaidi, hivyo juhudi ziwekwe kwenye mazungumzo kuutatua, na baada ya kuutatua yaendelee kufanyika mazungumzo ambayo yataleta suluhisho la kudumu kwa kuwa imekuwa ni kawaida kwa Zanzibar kuzuka migogoro kila baada ya uchaguzi mkuu jambo linaloonyesha kuwa tatizo ni la asili zaidi kuliko inavyodhaniwa.

Katika mazungumzo yake na wahariri hao wa New Habari Corporation Ltd, Wachapishaji wa magazeti ya Rais, Mtanzania na Dimba, alivitaka vyombo vya habari nchini, sasa kushirikiana na Serikali kulijenga taifa.

"Tunajua wakati wa kampeni kulikuwa na mambo mbalimbali ambayo wakati mwingine vyombo vya habari vililazimika kukampenia vinaowaona kuwa wanafaa kutokana na sababu mbalimbali, lakini kama tulivyokuwa tukisema, kwamba baada ya uchaguzi maisha yataendelea, sasa umefika wakati wa kuendelea na maisha tuwe kitu kimoja", alisema Nape.

Alivitaka vyombo vya habari, kusaidia kuishari Serikali na CCM, katika kutekeleza yaliyo bora kwa taifa na hata pale vyombo hivyo vitakapoona kwamba Chama au serikali vinaenda kinyume, visihofii kukosoa.

Kwa upande wao, Mtariri Mtendaji wa Habari Corporation, Absalom Kibanda akimpongeza Nape kwa ushirikiano ambao amekuwa akivipa vyombo vya habari, na kumtaka aendelee kuwacha milango wazi kwa waandishi wa habari kama ambavyo amekuwa akifanya.

Ziara hiyo ya Nape aliyoianza jana, kwenye vyombo vya habari inatarajiwa kuendelea kesho kwa kutembelea vyombo vingine vya habari vyenye makao yake makuu jijini Dar es Salaam.
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top