Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

BAADA YA KUFANYA MAHOJIANO NA SHOGA SASA WABUNGE WATAKA CLOUDS Tv IADHIBIWE


WABUNGE wameiomba serikali kukichukulia hatua kituo cha televisheni, Clouds Tv nchini kwa kukiuka maadili na taaluma ya habari kwa kurusha kipindi ambacho maudhui yake yalikuwa ni kutangaza mapenzi ya jinsia moja.


Mbunge wa Viti Maalumu, Amina Mollel (CCM) aliomba Mwongozo kuhusu kurushwa kwa kipindi ambacho kilikuwa kikimhoji kijana mmoja ambaye anajihusisha na vitendo vya ushoga.


“Napenda kuweka maslahi yangu kuwa mimi mwenyewe ni mwanahabari na taaluma hii naifahamu na ndio maana nikaona ni vyema nisimame angalau kupata muongozo wako,” alisema Mollel na kuongeza kuwa sheria ya nchi hairuhusu ushoga kwa maana hiyo kama mwandishi wa habari alipaswa kuzungumzia ushoga, basi angeelimisha jamii kwa kuonesha kuwa kijana huyo anajutia kufanya vitendo hivyo.


Alisema mwandishi huyo angefanya hivyo ili kutoa taarifa kwa wengine kwamba vitendo hivyo sio vizuri katika jamii badala yake kipindi kilihamasisha vitendo vya ushoga na alionesha ni mtu anayefurahia kitendo kile, na jambo la kusikitisha asubuhi hii (jana), mwendeshaji wa kipindi hicho alialikwa katika kipindi cha asubuhi cha kituo hicho, badala ya kuomba radhi ameishia kujitetea.


Kutokana na maelezo hayo, aliomba Mwongozo wa Spika pamoja na Kanuni na kwa kuwa serikali ipo, itoe kauli kama inaruhusu ushoga au kama hairuhusu ni hatua gani inachukua kwa kituo hicho ili iwe fundisho kwa vingine.


Naye Mbunge wa Viti Maalumu, Agness Maro (CCM) alisema kijana huyo aliyehojiwa na Kipindi cha Take One cha Clouds Tv amewaaibisha wakazi wa Musoma mkoani Mara, hivyo aliiomba serikali imchukulie hatua kwa sababu anaweza kuwafundisha tabia zisizofaa vijana wengine.


Naibu Spika, Dk Tulia Ackson akijibu miongozo hiyo, alisema jambo hilo linapaswa kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria zilizopo.

RASMI:MTANGAZAJI MASOUD KIPANYA AMEREJEA TENA CLOUDS FM

Kipanya
Mtangazaji Masoud Kipanya Jumatano hii April 27 2016 atasikika tena kama mfanya kazi wa CloudsFM atasikika kwa mara nyingine tena Masoud ambaye alipata umaarufu sana kupitia vipindi mbalimbali vya CloudsFM toka kitambo hicho.

CMG (Clouds Media Group) wamethibitisha hilo kupitia page ya Instagram kwamba Mtangazaji Masoud Kipanya anarejea kufanya kazi na atasikika kwenye show ileile ya POWER BREAKFAST akiungana na Barbara Hassan na Fredwaa ikiwa ni baada ya Gerald Hando na PJ kumaliza mkataba wao na CMG

RUGE AKANUSHA GERALD HANDO NA PJ KUACHA KAZI

12809737_1074835289226555_2108898734342699721_n
Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba.

MKURUGENZI wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba,  leo kupitia kipindi cha Power Breakfast‬ amekanusha uvumi wa watangazaji wa kituo hicho, Gerald Hando, Abel Onesmo na PJ,  kuacha kazi.

“Kwa nafasi yangu kama mkurugenzi,  taarifa nilizonazo ni kwamba tuna mikataba na wafanyakazi hao ambayo inaisha leo tarehe 31.  Sehemu kubwa ya wafanyakazi  wetu mikataba yao inaisha mwezi huu, hivyo  katika hali ya kawaida huwa tunatoa nafasi ya kumwambia anayetaka kuendelea na mkataba aandike barua au aseme,” alisisitiza Mutahaba.

RUGE MUTAHABA AZITAJA FURSA KUMI ZA KUZICHANGAMKIA

12677466_1249827545030585_2040709851_n[1]
Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group,Ruge Mutahaba leo amezitaja #FursaKumi kupitia kipindi cha Power Breakfast na Clouds360 cha Clouds Tv.
12783469_190002071367159_145537583_n[1]
“Kwanza anatakiwa kusikiliza #FursaKumi, lakini pili lazima ajitambue yeye, bila Nyota Ndoto kujua yeye ni mwanamuziki mzuri au ana kipaji cha kuimba leo isingefikia hatua ya msanii Nyota Ndogo kutoka, nadhani kikubwa wengi tunakosa kujitambua, kutojua tuna nini nguvu yetu ipo wapi naamini kila mtu ana kipawa na ‘talanta’ aliyozaliwa nayo “Alisema Ruge Mutahaba.
11355838_1130520630312010_118426074_n[1]
“Wengi hatujui ‘talanta’ tulizozaliwa nazo, kuna mtu anajua kuchora vizuri lakini hajawahi kufikiria kuwa ni ‘designer’ mzuri kwa sababu hakuna mtu aliyemsaidia kumwonyesha anaunganishaje hivi vitu ni kujaribu kujifunza kujitathimini, kujifahamu” Aliongeza Ruge Mutahaba.
12784126_484450141755989_984899504_n[1]
 “Tunaona madalali, ni madalali wa nyumba wangapi wanatumia ‘Instagram’ kufanya biashara zao, shughuli zao za kazi zote tunazozungumza ziko kwenye ‘contacts’ za simu, kwa kweli wanafanya kazi nzuri sana, ‘smart phone’ inafanya kila kitu kwa sasa hivi” Ruge Mutahaba


FURSA KUMI:
Fursa Namba 1: Biashara kwenye sekta ya Kilimo (Agri business). Kilimo ndio msingi wa kila kitu, Watanzania wengi wanalima ili wapate chakula ila si kwa ajili ya biashara. Jambo hili linatoa nafasi kwa watu kuweza kuwekeza kwani kupitia Kilimo tutakuwa na viwanda na watu wengi wataweza kujiajiri.



Fursa namba 2: Biashara ya Chakula (Food Business). Fursa hii naitazama kwenye kuongeza dhamani katika biashara na kuzidiwa kujitangaza, usipike tu kwa kawaida, ila ifanye kwa utofauti ikue na kuongeza kipato.



Fursa Namba 3: Biashara katika sekta ya Mauzo, Manunuzi ya rejareja na Usambazaji kupitia njia ya mtandao (Retail – E commerce). Unaweza kutumia mitandao kuuza bidhaa zako na kununua pia. Sio lazima ukutane na mteja ana kwa ana ila kupitia mtandao unaweza kuanza nguo, viatu na vitu vingine.



Fursa namba 4:Biashara katika tasnia ya Habari na Burudani(Media&Entertaiment. Tukiweza kutengeneza film bora zitasaidia kufikisha tasnia hii mbali. Nigeria wamerekodi filamu moja Marekani, ndani ya mwezi mmoja imeuza kopi laki 5. Na wakati wa sisi kuwekeza zaidi na zaidi ili tufikie huko.



Fursa namba 5: Biashara kwenye sekta ya Huduma za Kijamii. Kwa sasa Tunaona Hospitali na Shule nyingi za binafsi na zinafanya vizuri sana. Hi ni nafasi kwetu kuwekeza.



Fursa Namba 6 :Biashara katika Tasnia ya Mitindo na Urembo (Beuty &Fashion). zamani wote kwa mtazamo wetu mwonekano, mvuto ulitokana na fahari ya mtu mwenyewe alichozaliwa nacho, lakini katika ulimwengu wa sasa mwonekano wa mtu ni ‘featuring’ ya vitu vingi sana kuanzia nywele, kucha, make up, fursa zipo nyingi mf. Sasa hivi unaweza kuambiwa kufanya ‘pedicure & manicure’ ni shs elfu 40 hicho ni kimoja tu”Ruge Mutahaba



Fursa Namba 7: Biashara ya Mashamba, Majengo/Mali isiyohamishika (Real Estate). Tunaona Shule zinaongezeka na Vyuo pia. Hii inatoa nafasi kwa Watanzania kuwekeza kwa kujenga Hostel ambazo zitatoa huduma kwa Wanafunzi na ni kitu cha kudumu.



Fursa namba 8: Biashara katika sekta ya Usambazaji na Usafirishaji (Transport and Logistics).



Fursa namba 9: Sekta ya huduma za kifedha (Financial services) mfano ununuzi wa hisa. “Uelewa kuhusu masuala ya Hisa umekua sana na hii ni fursa nzuri sana kwa Vijana kama wataanza sasa kuwekeza katika Hisa”.



Fursa namba 10: Intaneti na Teknolojia. Mambo mengi sana kwa sasa yanafanyika kupitia mitandao. Watu wanaweza kufanya biashara kupitia mitandao Hii ni nafasi kwetu sisi kuweza kuwekeza. Hii itatupa nafasi ya kujiajiri na pia kwenda na wakati.

CHANZO:CLOUDS FM
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top