Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

Gesi Nyingine Yagundulika Bonde la Mto Ruvu....Ina Ukubwa wa Ujazo wa Futi Trilioni 2.17

Tanzania  imedhihirisha kuwa ni tajiri mkubwa wa rasilimali ya gesi asilia baada ya kugundulika kwa gesi nyingine katika bonde la mto Ruvu yenye ukubwa wa ujazo wa futi trilioni 2.17.

Ugunduzi huo wa gesi asilia umefanywa na Kampuni ya Dodsal Hydrocarbons and Power Tanzania Limited ambayo imekuwa inafanya shughuli za utafutaji wa gesi na mafuta katika Mkoa wa Pwani.

Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Pilavullathil Surendran alisema jana katika mkutano wa wawekezaji wa gesi na mafuta ulioandaliwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kuwa, thamani ya gesi iliyoko katika eneo hilo inafikia Dola za Marekani bilioni sita sawa na Sh trilioni 12.

Ugunduzi huo mpya unafanya hadi sasa Tanzania kuwa na amana ya gesi yenye ukubwa wa futi za ujazo trilioni 57.27.

Kwa upande wake, Profesa Muhongo alithibitisha kugundulika kwa gesi hiyo tangu Julai mwaka jana, lakini akaeleza kuwa Serikali imechelewa kutangaza ugunduzi huo kama inavyoagizwa na Sheria ya Mafuta ya Mwaka 2015 kutokana na shughuli za uchaguzi.

“Sheria mpya inatutaka kabla ya waziri mwenye dhamana ya gesi kutangaza ugunduzi mpya wa gesi na mafuta ni lazima athibitishiwe na mamlaka ya udhibiti wa bidhaa za Petroli na Gesi (PURA).

“Wizara yangu itawasiliana na mwanasheria mkuu wa serikali ili kupata ushauri wa kisheria kuhusu jambo hilo na bahati nzuri tayari PURA imeshaanza kushughulikia jambo hilo na naamini kuwa nitatangaza ugunduzi huo mpya hivi karibuni,” alifafanua Profesa Muhongo.

Licha ya ugunduzi huo mpya tayari gesi imegundulika katika maeneo ya kisiwa cha Songo Songo mkoani Lindi na eneo la Mnazi Bay huko Mtwara na katika Wilaya ya Mkuranga, Pwani pia kumegundulika kiasi kikubwa cha gesi.

Dk Kalemani atangaza neema kwa watumiaji umeme mdogo

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani akionesha Kifaa cha ‘Lead Board’ kwa viongozi wa Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma (hawapo pichani) hivi karibuni. Dk Kalemani alikutana na viongozi hao wakati wa ziara yake wilayani humo kukagua miradi ya umeme inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA). Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini, Peter Serukamba.
Fundi Umeme, akifunga umeme wa REA kama alivyokutwa na Msafara wa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani, eneo la Buselesele mkoani Geita hivi karibuni. Naibu Waziri alikuwa katika ziara ya kazi kukagua miradi ya umeme vijijini.

Na Veronica Simba - Kakonko

Serikali imesema, wananchi wa kipato cha chini, hususan wa vijijini, wenye nyumba zenye kuanzia Chumba kimoja hadi Vinne, wataunganishiwa umeme pasipo kutandaza nyaya za umeme (wiring) kwenye nyumba zao.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani, aliyasema hayo hivi karibuni Wilayani Kakonko, mkoani Kigoma, akiwa katika ziara ya kazi mkoani humo, kukagua miradi inayotekelezwa chini ya wizara yake, hususan ya umeme vijijini, kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

Dk Kalemani alisema, badala ya kutandaza nyaya za umeme katika nyumba zao, wananchi hao watafungiwa kifaa maalum kijulikanacho kitaalam kama ‘Lead Board’, kitakachowawezesha kutumia umeme kama kawaida.

Alisema, utumiaji wa kifaa hicho ni teknolojia mpya itakayowasaidia wananchi wa kipato cha chini kuondokana na gharama kubwa za kutandaza nyaya ndani ya nyumba, ambazo mara nyingi husababisha wengi wao kushindwa kumudu gharama hizo na hivyo kukosa huduma muhimu ya umeme.

Hata hivyo, Dk Kalemani aliweka bayana kuwa, watakaonufaika na huduma hiyo ni wale tu wenye kipato cha chini, wanaomiliki nyumba ndogo za kuanzia chumba kimoja hadi vinne. “Wenye nyumba kubwa wataendelea na utaratibu wa kawaida wa kutandaza nyaya.”

Alisema, Serikali imefikia uamuzi huo, baada ya kuona wananchi wengi wa vijijini, ambao kipato chao ni duni, wanashindwa kunufaika na huduma ya umeme, licha ya Serikali kuwapelekea huduma hiyo kwa gharama nafuu sana kupitia Mradi wa Umeme Vijijini unaotekelezwa na REA.

"Kama Serikali, tumedhamiria kuhakikisha asilimia 75 ya Watanzania wanatumia nishati ya umeme ifikapo mwaka 2025. Ili kufikia malengo hayo, ni lazima tuhakikishe tunawapatia huduma hiyo muhimu Watanzania wengi zaidi, na tuhakikishe wanawezeshwa kuitumia, hususani walioko vijijini, ambao wengi wao wana kipato cha chini,” alisisitiza Naibu Waziri.

Akifafanua zaidi kuhusu faida za kutumia kifaa hicho, Naibu Waziri alisema, wananchi watakaofungiwa ‘Lead Board’, watatumia shilingi 27,000 hadi 30,000 tu. Gharama hiyo inahusisha uwekaji wa nguzo, kuunganishiwa umeme nyumbani pamoja na kifaa husika.

Alibainisha kuwa, kimsingi, umeme wa REA ni bure, isipokuwa mwananchi analazimika kulipia shilingi 27,000 tu kama tozo ya kodi ya Serikali (VAT). “Tofauti na kulipia VAT, hakuna malipo hata Thumni kwani Serikali imegharamia umeme huo.”

Aliongeza kuwa, Serikali inaangalia utaratibu wa kuondoa hata shilingi 6,000 inayotumika kulipia fomu kwa ajili ya maombi ya umeme kama njia ya kumwezesha mwananchi wa kipato cha chini kutumia huduma hiyo.

Akizungumzia gharama za matumizi ya umeme, Dk Kalemani alisema, watumiaji wote wa umeme, ambao matumizi yao ni chini ya uniti 75, wanapaswa kulipia shilingi 100 tu za kitanzania kwa kila uniti moja. Alisema, gharama hiyo ni nafuu sana, hivyo hakuna sababu ya wananchi wa kipato cha chini kushindwa kutumia umeme kwani wako katika kundi hilo linalotumia umeme kidogo.

Dk Kalemani alifafanua kuwa, wapo baadhi ya wananchi wanaotumia umeme chini ya uniti 75, lakini kwa bahati mbaya, wamewekwa katika kundi la watumiaji wakubwa wa umeme, hivyo wanapaswa kupeleka malalamiko katika Ofisi za Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) katika maeneo yao ili wabadilishwe na kurudishwa katika kundi wanalostahili kuwa.

Vilevile, aliwataka viongozi katika ngazi mbalimbali, kuanzia Kijiji hadi Mkoa, kuelimisha wananchi juu ya matumizi bora ya umeme, kwani wengi wanatumia umeme vibaya na hivyo kulazimika kulipia bili kubwa.

Akizungumzia suala la kukatika-katika kwa umeme, Dk Kalemani alisema, Wizara yake imewaagiza Mameneja wa Tanesco wa Wilaya, Mkoa na Kanda nchi nzima, kuhakikisha wanarekebisha miundombinu mibovu ya umeme kama vile nguzo na transfoma ili kutatua tatizo hilo.

“Kwa hiyo, kukatika-katika kwa umeme kunakotokana na masuala ya kibinadamu, hakutarajiwi kuendelea baada ya Machi 31, mwaka huu.”

Aidha, aliwataka viongozi katika ngazi za Vijiji, Tarafa, Wilaya na hata Mkoa, kuhakikisha wanawasilisha majina ya vijiji ambavyo havikupangwa kupelekewa huduma ya umeme katika Mradi wa REA Awamu ya II, unaotarajia kukamilika ifikapo mwezi Juni mwaka huu, ili viingizwe katika Mradi wa REA Awamu ya III, unaotarajiwa kuanza mwezi Julai mwaka huu.

Alisisitiza kutokusahau maeneo muhimu kama Vituo vya Afya, Shule, Masoko, Magereza, Jeshi na mengine ya aina hiyo, ambavyo havikupangwa kwenye REA Awamu ya II, ili viingie katika REA Awamu ya III.

OIL AND GAS:OPEN LETTER TO MR.PRESIDENT JOHN POMBE MAGUFULI(CONCERNING OIL AND GAS)

TANZANIA MINES GAS/ENERGY AND OIL FORUM (TMGOF)
Media Department
TANZANIA MINES GAS AND OIL COMPANY LTD (TMGOL)
Registered Company
TMGOFLOGO_LARGE
TMGOF Centre of Extracts of Information for Extractive Industry
and
TMGOL Sponsor of Tomorrow in tapping Local Content Opportunities
18 January 2016
Dear
Mr. President John Pombe Magufuli
OPEN LETTER TO MR. PRESIDENT JOHN POMBE MAGUFULI
( CONCERNING OIL AND GAS )
Dear Mr. President Magufuli, Tanzania Mines, Gas and Oil Co. Ltd are 100% Tanzanian company with its own forum called Tanzania Mines, Gas/Energy and Oil Forum. Our mission is to promote our natural resources by organizing oil, gas and mines conference & Exhibition with the aim of being the sponsor of tomorrow economy in our country for the intention of tapping local content opportunities.
Mr. President you have demonstrated revered leadership in standing up for all Tanzanian. In moderation, I believe smart people, strategic plan can help us measure our progress in oil and gas sector today and in near future.
Mr. President in this Open letter I would like to share with you the story about the leader of a Middle Eastern nation was given a global competitiveness report showing that his country, despite being a major oil exporter, ranked very low in terms of global competitiveness. Investors were simply not prepared to invest in his country, except for a few dodgy characters. Foreign currency reserves were low, and young people were unemployed and roaming the streets.
First, he called in some senior politicians and asked what they thought of the report. Some said it was a hoax designed to embarrass the country. Others said it was the work of their enemies who wanted to steal their oil. Yet others said it was simply not true.
Then the leader quietly called one of the country’s leading business leaders. “Your Highness, do you really want to know the truth?” the man asked.  After listening to the business leader, the ruler of the country asked him to make recommendations to correct the situation. Using this “data,” they made bold changes to the laws of their country. Some laws in place for generations were simply repealed. The ruler retrained or removed civil servants and other regulators who were hostile to business and investment.
Mr. President you will be taking crucial decisions on the future of Tanzania in Oil and Gas for the benefit of Tanzanian and by considering climate change. Making the right choices now is critical to developing a policy that protects the climate and give chance Tanzanian to invest in oil and gas.
We would like to share with you some points that, we believe, will help in reaching such important decisions:
  1. There is the need for the TANZANIAN OIL & GAS SERVICE COUNCIL to represent the interests of Oil and Gas Service Providers in Tanzania with key mission to promote the capabilities of the Tanzanian Service Providers and showcase Tanzania as the regional hub for the Oil & Gas Industry. To achieve that, any policy should strive for technology neutrality and should phase out subsidies.
  • There is need to have country website and center unit for Oil and Gas which will help local investors to get all information in one place which will be under TANZANIAN OIL & GAS SERVICE COUNCIL. We believe this Council will run its activities independent without depend much in government fund.
  1. Choose one target and keep as the policy’s cornerstone. This Council may be one of the last chances to reconsider targets. This would be a significant step towards ensuring that gas plays a meaningful role in electricity production.
  • Gas emits roughly half the CO2 of coal: by taking one simple step policy – when calculating the emissions for the proposed natural gas power plants, please make the total as accurate as possible by including all emission sources — including those from natural gas extraction, production, processing, compression and delivery.
  1. Recognize the critical role that natural gas has to play in keeping the lights on: the more intermittent renewable energy comes on-stream, the greater the requirement for other energy sources which are capable of balancing them and guarding against a deterioration of supply security. Gas power plants are the best option available: they are reliable and flexible and in securing energy supply to keep citizens warm. With a fully integrated internal energy market, gas would be able to move freely throughout the Tanzania, improve Tanzania’s security of supply and contribute to greater energy efficiency.
  1. Recognize the contribution local of company and investors. There is the need for local investors to invest in this new sector whether by themselves or government support considering the factors of the country being powerfully economically.
  1. Support and facilitate more oil and gas exploration in Tanzania.
  • Tanzania still holds significant potential country in East Africa for this new sector of Oil and Gas: Current conditions have seen TPDC exploration activities with the good initiative to develop our country in this new sector.
  • To develop that untapped potential, we need predictable national fiscal and regulatory frameworks. While we should avoid unnecessary legislation, policies encouraging the role of oil and gas in the future Tanzania energy mix can help to trigger more investment – for the benefit of Tanzania’s security of supply, industrial competitiveness and economic growth.
We hope that these few points will help to enrich the discussion. We believe that they would move the Tanzania closer to reaching its goals, without drifting us & local investors away from the objective of a prosperous and sustainable. My team and I remain at your disposal for any further clarification you may want on any of these issues.
Respectfully,
Peter S. Hermes
Managing Director
Tanzania Mines, Gas/Energy and Oil Forum
Reg No: 114957
Email: peter.stephen@aiesec.net
Mobile: +255-755-503612
Website: www.tmgof.or.tz
Extension Media: www.tanzaniapetroleum.com

Cc:
Permanent Secretary
Ministry Of Energy and Minerals
P.O.Box 2000
DSM


Managing Director
Tanzania Petroleum Development Cooperation
P.O.Box 2000
DSM


Chairman of the TMGOL Board
Tanzania Mines, Gas and Oil Company Ltd
P.O.Box 54446
DSM

MAJI ya Mtera yatakiwa kutunzwa kwa mwaka mzima

Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo (wa kwanza kulia) akizungumza na watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mara baada ya kuwasili katika kituo cha kuzalisha umeme wa maji cha Mtera ili kukagua kituo hicho na kuzungumza na wataalam.Wa Tatu kulia ni Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli, Mhandisi Hosea Mbise), na wa Nne kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Sheria Wizara ya Nishati na Madini, Justus Mulokozi.
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo (katikati) akikagua kituo cha kuzalisha umeme wa maji cha Mtera mara baada ya kufanya mazungumzo na watendaji wa Tanesco wanaosimamia kituo hicho. Wa Kwanza Kushoto ni Kaimu Meneja wa Kituo cha Mtera, Eng. Manfred Mbyallu na kulia ni Meneja Uzalishaji Umeme wa Maji nchini, Antony Mbushi.
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo (wa kwanza kushoto waliokaa) akiwa katika chumba cha kuongozea mitambo ya uzalishaji umeme katika kituo cha kuzalisha umeme cha Kidatu mkoani Morogoro wakati alipofanya ziara katika kituo hicho. Katikati (waliokaa) ni Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli, Mhandisi Hosea Mbise na Wa Kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Sheria Wizara ya Nishati na Madini, Justus Mulokozi.
Muonekano wa Bwawa la Mtera kwa sasa, baada ya maji katika bwawa hilo kupungua kwa kiasi ambacho hakiruhsu umeme kuendelea kuzalishwa na kupelekea mitambo ya umeme kuzimwa tarehe 7 Oktoba, 2015.
Katibu Mkuu,Wizara ya Nishati na Madini,Mhandisi Omar Chambo (wa tatu kulia) akiangalia kiasi cha maji kilichopo katika Bwawa la Kidatu mkoani Morogoro ambapo kimepungua kutoka mita 450.00 hadi mita 439.48 kufikia tarehe 27 Novemba 2015.Wa kwanza kulia ni Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli, Mhandisi Hosea Mbise.
Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini (aliyevaa suti) akisikiliza maelezo kuhusu uzalishaji wa umeme katika bwawa la Kidatu mkoani Morogoro, wakati alipofanya ziara katika bwawa hilo. Anayetoa maelezo ni Meneja wa Kituo cha Kidatu, Eng. Justus Mtolera.
Kaimu Meneja Mwandamizi Uzalishaji Umeme wa Maji nchini, Lewanga Tesha (aliyesimama) akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo (katikati) kuhusu uzalishaji umeme wa maji nchini katika ziara ya Katibu Mkuu kwenye vituo vya Kidatu na Mtera.Wa kwanza kushoto ni Kaimu Meneja wa Kituo cha Mtera, Eng. Manfred Mbyallu.
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo (wa kwanza kushoto) akipata maelezo kuhusu kipimo kinachoonyesha kima cha maji katika bwawa la kuzalisha umeme la Mtera. Bwawa hilo lilisimamisha uzalishaji tarehe 7 Oktoba 2015 kutokana na kima cha maji kuwa chini ya kiasi kinachoruhusiwa kuzalisha umeme.Anayetoa maelezo ni Kaimu Meneja wa Kituo cha Mtera, Eng. Manfred Mbyallu (wa pili kutoka kulia).

VIONGOZI WIZARA YA NISHATI NA MADINI WAFANYA ZIARA LINDI NA MTWARA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo na Naibu wake, Mhandisi Paul Masanja pamoja na Kamishna wa Nishati, Mhandisi Hosea Mbise hapo jana walifanya ziara kwenye maeneo mbalimbali yanayopitiwa na mradi mkubwa wa Gesi Asilia.

Lengo kuu la ziara hiyo ni kujionea shughuli zinazoendelea kwenye mradi wa gesi asilia pamoja na kuzungumza na wafanyakazi wa maeneo hayo kuhusu masuala mbalimbali ya shughuli zao za kila siku.

Maeneo ambayo yalitembelewa na viongozi hao ni pamoja na Kituo cha Kupokea Gesi Asilia ya Mtwara na Lindi cha Somangafungu (Somangafungu Gas Receiving Station) kilichopo wilayani Kilwa, mkoa wa Lindi; Visima vya gesi asilia vya Mnazi Bay na Msimbati; Sehemu iliyoathiriwa na Mmomonyoko wa ardhi ya Msimbati na Kituo cha Kuchakata gesi asilia cha Madimba cha mkoani Mtwara.

Wengine katika ziara hiyo ni Kamishna Msaidizi wa Nishati sehemu ya Gesi Asilia, Mhandisi Norbert Kahyoza, Meneja wa Kampuni ya Gesi Asilia (GASCO), Mhandisi Kapuulya Musomba na Maafisa kutoka Wizara ya Nishati na Madini.

Ziara hiyo ni miongoni mwa mikakati iliyowekwa na viongozi hao kukagua shughuli mbalimbali za masuala ya Nishati na Madini kote nchini.
Baadhi ya mitambo katika Kituo cha Kupokelea Gesi Asilia kutoka Songosongo na Mtwara kilichopo Somangafungu wilayani Kilwa Mkoani Lindi
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo (kulia) na Naibu wake, Mhandisi Paul Masanja (kushoto) wakimsikiliza Meneja wa Kampuni ya GASCO, Mhandisi Kapuulya Musomba (hayupo pichani) akiwaeleza kuhusu Kituo cha Kupokelea Gesi cha Somangafungu. Katikati ni Msimamizi wa Kituo hicho, Mhandisi Msafiri Peter.
Baadhi ya mitambo ya kupokelea gesi asilia iliyopo kwenye maeneo kilipo kisima cha gesi asilia cha Mnazi Bay Namba 3.
Sehemu ya Mitambo ya kuchakata gesi asilia ya Madimba inavyoonekana wakati wa usiku. Kituo hicho cha Madimba kilitembelewa na viongozi hao na kujionea shughuli zinazoendelea kituoni hapo.
Sehemu ya eneo lililokumbwa na Mmomoyoko wa ardhi uliotokea Mwezi Januari mwaka huu katika kijiji cha Msimbati baada ya mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali kunyesha katika maeneo hayo. Katika eneo hilo bomba kubwa la gesi asilia linakatiza kuelekea kwenye kituo cha kuchakata gesi asilia cha Madimba.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo (wa sita kutoka kushoto) na Naibu wake, Mhandisi Paul Masanja (kushoto kwake) wakiwa katika picha ya pamoja na wataalamu wengine mara baada ya kutembelea kisima cha gesi asilia cha Mnazi Bay namba 3 (MB 3).

BAADA YA KASI YA RAIS MAGUFULI,KATIBU MKUU WIZARA YA NISHATI NA MADINI ATAKA KAULI ZA ''NJOO KESHO'' ZIKOME MARA MOJA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo (kushoto) akijadiliana jambo na Kamishna wa Nishati, Mhandisi Hosea Mbise (katikati). Wa kwanza kulia ni Kamishna Msaidizi anayeshughulikia Maendeleo ya Nishati, James Andilile.
Wajumbe wa kikao wakimsikiliza katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo.
Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Felix Ngamlagosi (kushoto) akizungumza wakati wa kikao na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo (kulia). Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi- EWURA, Profesa Jamidu Katima.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo (kulia) akipokea nyaraka mbalimbali kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi- EWURA, Profesa Jamidu Katima. Anayeshuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Felix Ngamlagosi.

Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati na Madini zimeagizwa kutochelewesha kushughulikia maombi ya wawekezaji pale wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi wanapoonesha dhamira ya kuwekeza. Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo ametoa agizo hilo hivi karibuni wakati wa kikao chake na Watendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi hiyo.

Mhandisi Chambo aliwaagiza watendaji hao kuacha kufanya kazi kwa mazoea, na badala yake wazingatie Sheria na maadili ya kazi zao, kutokana na ukweli kwamba sekta ya Nishati ni sekta nyeti inayohitaji watendaji waadilifu na wabunifu.

“Akitokea mwekezaji ambaye ameonesha nia ni vema ajibiwe haraka bila kuchelewa iwe amekubaliwa au kukataliwa ombi lake; hakuna sababu ya kumzungusha mwekezaji; tuzidishe kasi ya uwajibikaji,” alisema Mhandisi Chambo.

Alisema lengo la Serikali ni kuongeza uwekezaji hususan kwenye sekta za Nishati na Madini na hivyo hakuna sababu ya kuchelewesha uwekezaji kwani fursa za uwekezaji zilizopo nchini ni nyingi.

Aliwaasa EWURA na Taasisi nyingine kuacha tabia ya woga, na kusema kwamba endapo itatokea mwekezaji akatuma maombi ya kuwekeza nchini, wanapaswa kupitia maombi husika, kujiridhisha na kutoa maamuzi kwa haraka na kwa kujiamini.

“Tufikie mahali tufanye maamuzi. Msiwe na woga kwenye kutekeleza jambo lenye maslahi mapana ya Kitaifa; majibu ya njoo kesho hatutayavumilia,” alisema.

Vilevile Mhandisi Chambo alisema ni vyema taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati na Madini zikashirikiana na Wizara katika kufanya upembuzi yakinifu wa miradi katika maeneo ambayo yanahitaji uwekezaji. Aidha, aliwaagiza watendaji kukaa pamoja kujadili maeneo ya kipaumbele ili upembuzi yakinifu ufanyike kwa lengo la kurahisisha majadiliano na wawekezaji.

Alisema ni vyema ikaundwa timu ya wataalamu kutoka katika Taasisi na Wizara ambao watahusika moja kwa moja na suala la kubaini maeneo pamoja na kufanya upembuzi yakinifu kwa miradi yenye tija na manufaa na hivyo kufikia mwafaka mapema na kuanza utekelezaji wa mradi husika pale mwekezaji anapojitokeza.

“Ikitokea mwekezaji akaonesha dhamira ya kuwekeza kwenye maeneo husika ni vema taarifa za awali zikawepo. Hii itavutia wawekezaji wengi zaidi lakini pia itaharakisha majadiliano,” alisema. Aidha, Mhandisi Chambo aliwapongeza EWURA kwa kufanya vizuri kwenye masuala ya mafuta na kuwaasa kujitahidi kufanya vizuri katika majukumu mengine yaliyo chini yao. Naye Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Felix Ngamlagosi aliahidi kufanya kazi kwa uadilifu na kuzingatia maelekezo yaliyotolewa na Katibu Mkuu pamoja na kumpatia ushirikiano wa kutosha. Kikao hicho ni mwendelezo wa vikao vya Katibu Mkuu huyo na Menejimenti pamoja na Bodi za Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati na Madini ili kupata ufumbuzi wa changamoto zinazozikabili.
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top