Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

Mchungaji Obadia atumia Mkanda na Chupa ya Maji kuvutia Watu ili Wasikilize Mahubiri yake.

Anaitwa Mchungaji Obadia akiwa anatangaza neno la Mungu maeneo ya Soko La Karume na hao ni baadhi ya watu waliokuwa wakimsikiliza Mchungaji huyo ambae ni mwenyeji wa Mkoa waKIlimanjaro kama alivyokuwa anasema na amewahi kukaa nchini Kenya kwa Muda wa Miaka Kumi kabla ya kuamua kurudi nchini.
Hapo anaonyesha mkanda ambao ameuweka chini kama unavyoona pembeni ya chupa ya maji hapo ambao aliutumia kuwavutia watu waje kuona miujiza atakayotenda hapo kwa maji kugeuka rangi hali iliyofanya kila mmoja awe na shauku kusubiria miujiza hiyo.
Baadhi ya watu wakiwa wanasikiliza kwa makini neno la Mungu toka kwa Mchungaji Obadia pia wakiwa na shauku kubwa kujua miujiza hiyo ya Mkanda wa suruali na chupa ya Maji ni upi huo hivyo kukaa kwa makini kabisa kusubiria huku wakichapwa neno la Bwana.

Anaonekana akipokea sadaka toka kwa mmoja wa watu waliokuwa wamehudhuria mkutano huo wa Injnili wa Mchungaji Obadia hapo Karume soko la Mitumba.Watu wakionekana wamekaa kusubiria miujiza ya Mchungaji huyo Obadia.

Lakini kilichowaacha watu hoi ni Pale Mchungaji huyo alipoanza kusema tumekuwa watu wa jabu sana hatutaki kusikiliza neno la Mungu badala yake tumegeuka watu wa kupenda kuona Miujiza
Akazidi kusema'' Kama leo nimeanza kuhubiri hapa hakuna mtu alitaka kuja kusikiliza nikaona watu wanapita tu wananiaangalia nikafikiria nikaona ngoja niweke mkanda hapa na hii chupa ya Maji ili niwaambie nitatenda miujiza na kweli mmekaa na kusubiria miujiza hiyo Na Hapa hakuna miujiza mmekuja mmesikiliza neno la Mungu Bwana asifiweeeeee !!!!!''' Baada ya kumaliza kusema hayo alichukua mkanda na kurudisha kwa kijana wake na maji kuyaweka juu ya gari .
Watu tulikokuwa tunamsikiliza sasa tuakabaki na vicheko huku wakimsifu kwa mbinu hiyo aliyotumia na kila mmoja kuondoka huku anafuraha tele !!!

Huyo alikuwa Mchungaji Obadia
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top