Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

Mh.Anna Kilango Malecela ang'aka kuhusu uharibifu wa Msitu wa Shengena


Mh.Anna Kilango Malecela akiongea Muda mfupi uliopita Bungeni ameshangazwa na mamlaka zinazohusika kufumbia macho uharibu wa mazingira unaofanyika katika Msitu wa Shengena hata kusababisha wa vyanzo vya maji navyo kuharibika.
''Uharibifu wa Msitu wa shengena umevamiwa na Majangili yanayovuna dhahabu kwa kuharibu msitu huo unaotegewa na mito ya Safeni,Hingilili,Nakombo na Shengena hivyo kufanya maji eneo hilo kukauka kwa kisa hicho cha majangili'' alisema Mh.Kilango.

Pia alitaja Madhara yanayotokana na uharibifu huo kuwa ni Pamoja :
-miaka miwili wamekuwa wakitumia maji yenye kemikali
-mvua zimepungua
-mito inatiririsha maji mekundu kutoka msitu huo.

Ameiomba Serikali kufanya yafuatayo Mara moja:
-kusimamisha uharibu unaofanyika katika msitu shengena mara moja
-Kuurudisha kama mwanzo msitu wa Shengena.

Akaongeza kuwa Wananchi wa Same wanaandaa utaratibu wa kwenda UNO kuhusu suala la msitu wa Shengena LAKINI akawaomba wananchi hao kuachana na wazo hilo kwani yeye atashughulikia kwani haogopi mtu.

Ashangazwa na ukimya wa Waziri alienda eneo hilo la Msitu wa Shengena mwaka 2010 kuwa kimya mpaka sasa huku uharibifu ukiendelea mpaka sasa.

Aliongeza kuwa Wananchi wamekunywa sumu kwa miaka 2 kutoka msitu Shengena.

Source Arusha Mambo FM ''LIVE'' online
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top