Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

Zitto Kabwe:Tutaendelea kutayarisha Bajeti Mbadala, Ndio Upinzani Makini



Kumekuwa na mada mbalimbali kuhusu mapungufu ya kihariri kwenye Bajeti Kivuli ambayo Kambi ya Upinzani iliandaa na kuwasilisha Bungeni.

Kwa niaba ya wenzangu tulikiri mapungufu haya na kuoomba radhi kwa usumbufu uliotokea. Kwa niaba ya wenzangu wote ninawajibika kwa jambo hili kwani mimi ndio mwenye mamlaka ya mwisho ya kuwasilisha Hotuba yetu kwenye Baraza la Mawaziri Kivuli na hatimaye Bungeni. Ninawajibika mapungufu yote yaliyotokea. Ninaahidi kwamba tutaboresha zaidi miaka inayokuja.

Kulikuwa na makusudi kwenye mapungufu?

Hapana. Utaona kwamba nambari ambazo hazikuwekwa kwenye Jedwali zilikuwepo kwenye hotuba. Kosa ilikuwa ni kusahau kuhamisha nambari za vyanzo vya mapato ambazo viliweza kufikia tshs 11tr tulizoweka kama mapato ya ndani. Sio kweli kwamba tuliweka Mapato Sifuri. Mapato yote ya ndani ya Serikali tuliweka jumla yake na kusahau kuweka vyanzo kama Mapato ya kikodi, mapato yasiyo ya kikodi na mapato ya halmashauri. Tulipoona mapungugu hayo tulikrekebisha mara moja. Hapakuwa na makusudi yeyote isipokuwa tunfanya kazi kwenye mazingira magumu sana. Waziri Kivuli wa Fedha anasaidiwa na kundi dogo la 'interns' na wataalamu wengine walio nje ya Bunge. Hivyo kosa kama hili la kiuhariri linaweza kutokea. Tumezingatia hasira za wanachama na wapenzi wetu na hivyo tunaahidi kwamba tutaangalia kwa kina zaidi hotuba zetu zinazofuata.

Hakuna haja ya kuwa na Bajeti Mbadala?
Upinzani wowote makini lazima uwe na uwezo wa kutoa mawazo tofauti, hatuwezi kuwa watu wa kulalamika tu bila kuonyesha sisi tungefanya nini. Tumekuwa tunatoa Bajeti Mbadala kila mwaka tangu mwaka 2007 na mafanikio yamekuwa makubwa sana.

Tumeboresha hotuba zetu mwaka hadi mwaka na hoja zetu zimekuwa zikichukuliwa na Serikali kuboresha Mapato. Changamoto kubwa sana tuliyonayo ni namna bora ya kusimamia uwajibikaji katika matumizi ya Serikali ambayo yanakua siku hadi siku.

Mwaka jana katika Bajeti mbadala, tulishauri kuhusu tozo ya SDL itumike kugharamia elimu ya Juu. Serikali ilichukua wazo hili. Mwaka huu tumependekeza kwamba tozo hii pia itolewe na Mashirika ya Umma, Serikali imekubali. Mabadiliko haya yataingiza zaidi ya Tshs 320bn na kuweza kulipia mikopo wanafunzi takribani 120,000 ikiwemo fedha kwa ajili ya VETA.

Mwaka jana katika Bajeti mbadala tulipendekeza kutunga sheria kuzuia makampuni makubwa ya nje yanayouziana 'assets' zilizopo Tanzania bila kulipa kodi. Mwaka huu SeLinkrikali imetekeleza wazo hili. Kuanzia sasa mauzo ya rasilimali zetu yaliyokuwa yanafanywa holela sasa yamezuiwa kisheria. Changamoto ni utekekezaji kutokana na ufisadi uliokithiri katika mfumo wa Serikali na wakusanya mapato.

Kuna jumla ya mapendekezo 10 katika Bajeti Mbadala ya mwaka huu yamekubaliwa na Serikali. Tunatendelea kutoa mawazo zaidi ili kuboresha nchi yetu na kuwaonyesha Watanzania kuwa tukikabidhiwa dola tunaweza kuendesha nchi bila mashaka yeyote.
SOMA ZAIDI JAMII FORUMS PAMOJA NA MAONI MBALIMBALI
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top