Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

Imeng'ang'ania Madaktari wanataka fedha, Je! haya mengine mbona hamyasemei?

Madaktari waliporudi kazini mwezi wa pili niliandika kuitahadharisha serikali kwamba, ingawa madaktari wamerudi kazini, mgomo wao haujaisha. Watu ambao mioyo yao imepondekapondeka kurudi kazini hakuwezi kumaliza tatizo.

Ni bahati mbaya kuwa makosa yaliyofanyika katika kumaliza mgomo mara ya mwisho yanajirudia. Vitisho na kutishia ni dalili za mtu aliyepoteza mwelekeo katika mapambano.

Huwezi kujivunia madaktari wa Jeshi ambao nao wana wagonjwa wao wa kutosha. Madaktari wa Jeshi hawagomi, lakini ni mshahara upi mkubwa kati ya ule wa kijeshi na wa udaktari?

Waliojenga hospitali za serikali wakatenga kuwa hizi zitumiwe na jeshi na hizi zitumiwe na raia walikuwa na fikra kubwa. Una akili gani kutaka kuuvuruga utaratibu huo? Ni kupotoka kunakoashiria maafa zaidi kwa raia na kwa wanajeshi pia.

Je, siyo kweli kuwa ukiwajumlisha madaktari wote, wanajeshi, wa hospitali binafsi na hawa waliogoma nchi bado ina upungufu wa madaktari? Unazibaje upungufu kwa kutumia upungufu? Viongozi wetu wanahangaika sana huku wakifanya kazi ya bure.

Umri wa kustaafu ukifika mtu aliyechoka anapumzika. Kuna akili gani kumrudisha mchovu shambani? Hao madaktari wa kigeni wanaletwa kujitolea? Hawatalipwa?

- Madaktari wanadai vitendea kazi.
- Wamechoka kuona wagonjwa wakifariki kwa kukosa hata oksijen tu!
- Wamechoka kuwalaza wagonjwa chini au kuwalundika katika kitanda kimoja wenye magonjwa tofauti tofauti.
- Wamechoka kuwaandikia wagonjwa dawa ambazo hazipo hospitalini lakini kwenye Bohari Kuu ya madawa zipo.
- Wanadai wanaohusika na ununuzi wa mitambo ya kitabibu kwa bei mbaya, lakini mibovu waondolewe.
- Wanaoruhusu madawa feki waondolewe.

Haya mbona hayasemwi na serikali? Imeng’ang’ania moja tu, madaktari wanataka fedha.

Kuagiza madaktari kutoka nje, hao madaktari watakuja na vitendea kazi vyao? Wataleta madawa yao, vitanda vyao na vifaa vingine? Kesho walimu watakapogoma tutaagiza walimu kutoka nje?

Busara iko wapi hapa?

Tukiendekeza fikra mufilisi kama hizi iko siku tutajikuta tunaagiza hata Rais kutoka nje!

Paschally Mayega
0713 334239

MwanaHalisi
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top