Michuano ya Kombe la Kagame leo inaingia katika hatua ya nusu fainali huku wenyeji Tanzania ikiwakilisha na kwabu mbili za Yanga na Azam Fc.
Katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali timu ya Azam FC itaumana na Vita Club kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.
Azam FC Vs AS Vita, Nusu Fainali Kagame Cup, Wanaoanza leo ni
1. Deogratius Munishi GK (27)
2. Ibrahim Shikanda (21)
3. Erasto Nyoni (6)
4. Aggrey Morris (13) Captain
5. Said Moradi (15)
6. Jabir Aziz (25)
7. Kipre Tchetche (10)
8. Ibrahim Mwaipopo (4)
9. John Bocco(19)
10. Salum Abubakar (8)
11. Ramadhan Chombo (17)
Wakati katika mchezo wa pili mabingwa watetezi wa Kombe hilo timu ya Yanga itashuka dimbani kutafuta nafasi ya kucheza fainali itakapo pambana na timu ya APR ya Rwanda.
Mwaka jana Yanga ilitwaa ubingwa wa michuano hiyo inayoandaliwa na Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) baada ya kuwafunga mahasimu wao timu ya Simba kwa bao 1-0.
Mabingwa watetezi Yanga ambao leo katika mchezo unaotazamiwa kuanza saa kumi watarusha karata zao watakapochuana na APR ya Rwanda katika mchezo unaotazamiwa kuwa wa kukata na shoka.
.............................................
Tunawatakia kila la kheri wawakilishi hao wa Tanzania katika michezo yao Leo
...................................................
UPDATE;AZAM VS VITA
DK 35: AZAM 0 - 1 AS VITA (kafunga Alfred
Dk ya 60 VITA CLUB 1 AZAM 0 RED Card kwa mchezaji Vita
AZAM 1 VITA 1 Dk 68 ( Bocco)
Kipindi cha pili chaanza, Mshambuliaji John Boko awainua mashabiki wa Azam FC na Watanzania kwa kusawazisha bao.Mpira unaendelea
DK 89: Azam Fc 2 (Mrisho Ngassa)- 1 As Vita
Mrisho Ngasa awainua tena mashabiki wa Azam na Watanzania kwa kupachika bao la pili dhidi ya AS Vita.(2-1)
FT: Azam FC 2-1 Vita
Mpira Umekwisha Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam Azam yaichapa As Vita 2-1
Post a Comment