Korea Kusini wagomea mechi ya Olimpiki
Timu ya kandanda ya wanawake kutoka Korea kaskazini waliondoka uwanjani kabal ya mechi ya ufunguzi ya mashindano ya Olimpiki mjini London baada ya ya bendera ya Korea kusini kupeperushwa kimakosa kando ya majina ya wachezaji katika runinga ya uwanjani.
Mechi hio dhidi ya Colombia katika mji wa Glasgow ilicheleweshwa kwa zaidi ya saa moja.
Mechio hio iliendelea baada ya waandaji wa michezo hio ya Olympiki kuomba msamaha, na Korea Kaskazini wakashinda kwa mabao mawili kwa nunge.
Kumwkuwa na uhasama kati ya Korea kusini na Kaskazini tangu kusitishwa vita dhidi ya nchi hizo mbili manmo mwaka wa 1953.
Chanzo:BBC Swahili
...........................................................................
Baadhi ya Picha zikionyesha tukio Hilo lilivyokuwa.
Afisa wa Timu ya Korea Kaskazini Son Kwang Ho akiwaelezea maofisa wa Olyimpiki inakuwaje bendera hiyo ya Korea Kusini kuwa sambasamba na majina ya timu yetu ya Korea Kaskazini.Hali ambayo maofisa hao waliomba radhi kwa kitendo hicho.
Mashabiki hao wa Korea Kaskazini wakibaki vinywa wazi kwa kushangaa kitendo hichoi cha bendera ya Korea Kusini kuonyeshwa hapo badala ya Korea Kaskazini.
Wachezaji wa Korea Kasakazini wakiwa wameondoka Uwanjani baada ya kubaini kosa hilo baadae walikubali kuingia tena Uwanjani.
Kikosi cha Timu ya wanawake ya Korea Kaskazini kikiwa tayari kwa mpambano.
Bendera ya Korea Kaskazini ikiwa imewekwa kwenye skrini kubwa uwanjani
Wakishangilia baada ya kushinda mechi yao na Colombia kwa mabao mawili kwa nunge.
Post a Comment