
HOTUBA YA MSEMAJIMKUU WA KAMBI YA UPINZANI MHESHIMIWA VINCENT JOSEPHAT NYERERE (MB), KUHUSUMAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA WA FEDHA 2012/2013 WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
Imezuiwa kwa muda kusomwa bungeni ili iweze kujadiliwa kwani kwa mujibu wa Spika imegusia Kesi ambazo ziko mahakamani.
Lakini Mh.Tundu Lissu anasema:Tumetaja masuala ya vifo vya kisiasa na si masuala yaliyopo mahakamani!Wataje kesi namba,wahusika
Akadakia Mh.Lukuvi:All issues found in pg3-5 touches matter in court.They have to be removed first before submission.
Nae Mwanasheria Mkuu akiongezea ...
AG,Werema:Chief whip wa Opp.anaongoza kwa kutokuwa na nidhamu.Na ushahidi amevunja sehemu ya meza yake.
Na Kesi zinazoongelewa ni Kesi zilizopo Katika hotuba ya Waziri Kivuli,V.Nyerere ambazo zisisomwe; 1.Dr.Ulimboka 2.Mch.Msigwa 3.Highness(MB):kujeruhiwa.
Alipopewa nafasi aongee Mh.Cheyo alisema:Tunaomba watu watoe hoja kwa utulivu bila hata kuvunja madeski.
Ndipo Spika akatoa maagizo..
Mh.Makinda:Sehemu ya mauaji ya kisiasa yarukwe!Tutaenda kufatilia.Tukirudi kama haina shida utawasilisha.Ruka mpaka uk.7
Makinda:Nimeshaamua.Aruke,na aendelee uk.7!Kamati ya maadili itapitia uk 3-6 na kujiridhisha kama yanaweza kusomwa Bungeni.
Baada ya Maagizo hayo ya Spika ,Mh.Lissu ameomba muongozo...
Lissu: Muongozo; Kwanini watoa hoja wengine wakitoa hoja hawakatishwi ila wa upande wa wachache wanakatishwa na kuzuiwa kusema?
Post a Comment