Yametokea mashambulizi kwenye makanisa mawili Kaskazini Mashariki mwa Kenya katika mji waGarissa leo hii Jumapili.
Mkuu wa upelelezi nchini Kenya Muhoro Ndengwa ametabainisha kuwa watu waliouawa ni nane huku Maafisa wawili wa Polisi nao wakiuawa ambao walikuwa wakilinda maeneo hayo ya ibada katika kanisa la katoliki na lile la Afrika Inland Church(AIC).
Huku wakitumia magruneti mawili waliyorusha juu ya kanisa yaliyojeruhi watu zaidi huku washambbuliaji hao wakikimbia baada ya mashambulizi hayo.
Kumekuwa vikitokea visa vya mara kwa mara nchini Kenya toka nchi hiyo ilipoanza kuwafurumusha wana mgambo wa Al-Shabaab ndipo wapiganaji hao walipoazimia mashambulizi zaid.Mpaka sasa hakuna kikundi kilichodai kuhusika na shambulizi hilo.
Vyanzo vya habari hii ni Daily Nation na The Standard
.
Post a Comment