Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

Taswira:Hapa na Pale Jijini Dar es Salaam

Ubungo pembeni mwa Barabara ya Mandela mitambo ya Umeme SONGAS ikionekana kwa mbali hapo huku vijana wa bodaboda wakiwa makini kabisa kusubiria abiria hapo kuelekea maeneo mbalimbali jijini hapa.Sehemu hiyo imekuwa nyeupe bila wafanyabiashara waliokuwa wakifanya kazi maeneo hayo na kuwa na msungamano mkubwa,baada ya kuondolewa hali ni kama uonavyo Wazee wa Bodaboda wakivinjari.

Jamaa akipatia magazeti kidogo ili aweze jua nini kinaendelea.Ni mfanyabiashara huyo ''machinga'' akiwa kaweka bidhaa zake juu ya bega akiperuzi habari kwa chati ili awahi kutafuta wateja mbele kwa mbele.Hapo ni maeneo ya barabara ya kuingia ofisi za TANESCO Magomeni ukitokea barabara ya Morogoro.
Wazee hao waweza sema ni ''wazee wa chabo'' wakiangalia mazoezi ya mpira wa miguu ndani ya viwanja vya Shule ya Sekondari ya Benjamini W.Mkapa yaliyokuwa yanaendelea baiskeli ikiwa pembeni.

Pembeni mwa Mtaa wa Msimbazi vijana vijana wakipiga mzigo kama kawa.Ni wauza matunda hao wakisubiri wateja.Jamaa nae sijui kimemsibu nini tena ? au ukishiba tena watakiwa uguseguse kitambi ? Au ndio hizi fasheniii..!! Brazaa Kaka shushaa Fulana wateja tununue matunda.
Jamaa anapiga mzigo pembezoni mwa mtaa wa Msimbazi Kariakoo.Hapo wakitokea mgambo yeye anakinyanyua tu kiduka chake bila wasi na anatokomea umekuwa ni kama mchezo wa paka na panya kati ya Machinga hao na Mgambo wa Manispaa zetu kwani imekuwa wanakimbia wakiwaona kwa mbali wakipita wanarudi mzigo kama kawa.
Wale wa Tabata Segerea hii ni Barabara ya kuingia Bunyokwa Segerea ukiiacha barabara ya kwenda Kinyerezi.

Taswira hizo zikionyesha Barabara ya kwenda Kinyerezi ukitokea Tabata Segerea ikionekana maridadi kabisa kwa mandhari ya kuvutia

Wazee wa Chuma chakavuu Mpoo !!!
Ni pembezoni mwa daraja linalo unganisha Tabata Segerea na Kinyerezi kuna magari hayo yalikuwa kwenye gereji ambayo iko mbele ya hili daraja yalisombwa na maji kipiindi cha mafuriko yaliyotokea Jijini Dar es Salaam na kuvunja madaraja kadhaa likiwemo hili linalounganisha Segerea na Kinyerezi.
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top