

UPDATE:Toka Uwanja wa Taifa
Dakika 22' Hamisi Kiiza alishacheka na nyavu lakini anaambiwa alikuwa ameotea
Dakika ya 30, Young Africans 0 - 0 Mafunzo FC
Dakika ya 34, Ally Othman Mbanga anaipatia Mafunzo bao la kwanza
HALF TIME: YANGA 0-1 MAFUNZO
Dakika ya 46, Said Bahanunzi anaipatia Young Africans bao la kusawazisha. Young Africans 1 - 1 Mafunzo FC
Dakika ya 51, Young Africans inafanya mabadiliko, anaingia Jeryson Tegete anatoka Rashid Gumbo
Dakika 60: Yanga wamekuja na kasi kipindi cha pili, safu yake ya ushambuliaji inaonekana kuwa na uchu wa mabao
Dakikaya 64, Young Africans inafanya mabadiliko, anaingia Idrisa Rashid anatoka Stephano Mwasika
Dakika 69: Limepigwa shuti kali na limepanguliwa kwa ustadi na kipa wa Yanga Berko na kubaki majeruhi
Dakika 70: Shuti limemuacha Yew Berko akiwa majeruhi na sasa anaingia Ally Mustafa Barthez
Dakika ya 75, Young Africans 1 - 1 Mafunzo FC
Hamis Kiiiza anakosa bao la wazi dakika ya 77
Ball possesion Mafunzo 54 Yanga 46
Dakika 83: Yanga 1-1 Mafunzo
Dakika 83: Mafunzo: Anatoka Salum Shebe anaingia Kheir Salum Kheir
Dakika ya 86,mpira umesimama kwa muda mchezaji wa Mafunzo amepoteza fahamu
Ali Othman Mmanga wa Mafunzo ametolewa nje kwenye machela baada ya kujeruhiwa
Dakika 90: Zimeongezwa dakika 5 za nyongeza
Mafunzo wamecheza dakika 6 za mwishoni wakiwa pungufu baada ya kuwa wamemaliza sub zao zote
Mpira umemalizika, Young Africans 1 - 1 Mafunzo FC
Mshindi sasa kuamuliwa kwa matuta
PENATI:
Goal: Bahanuzi anafunga penati ya kwanza 1-0Salum Said Shebe anafunga kwa upande wa mafunzo 1-1
Nadir Haroub Cannavaro anafunga kwa upande wa Yanga 2-1
Said Mussa Shaaban anakosa kwa upande wa mafunzo. Yanga wanaongoza 2-1
Hamis Kiiza anafunga kwa upande wa Yanga na sasa wanaongoza 3-1
Mafunzo wanafunga penati yao ya nne na sasa ni 3-2
Haruna Niyonzima anafunga kwa upande wa Yanga. 4-2
Juma Jaku anafunga kwa upande wa mafunzo 4-3
Athuman Idd Chuji anaipeleka Yanga nusu fainali baada ya kufunga penati ya mwisho kwa upande wa Yanga
Young Africans imeingia nusu fainali, baada ya kufunga penati 5-3 Wafunagji: Bahanunzi, Cannavaro, Kiiza, Niyonzima na Chuji
4 comments
Hongera YANGA kwa kuifunga MAFUNZO
ReplyTunawasubiria nyie ndala tuwafundishe ball kesho sie tunaisambaratisha Azam warudi Chamazii haraka....Yanga tunakuja SIMBA ngriiiiiiiiiiiiiiiii
ReplyNani alifunga penalti ya tatu ya Mafunzo? Hamjasema
ReplyJuma Jaku anafunga anafunga kwa upande wa Mafunzo 4-3
ReplyTunashukuru kwa kufuatilia kwa karibu Rundugai Blog
Post a Comment