Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

YANGA YAINGIA NUSU FAINALI,BAADA YA KUIFUNGA MAFUNZO KWA MATUTA

Mchezaji wa timu ya Yanga Stefano Mwasika akikokota mpira kuelekea goli la timu ya Mafunzo ya Zanzibar huku beki wa timu ya Mafunzo Ismail Khamis Amour wakati timu hizo zikichuana katika mchezo wa Robo Fainali ya Kombe la Kagame unaofanyika jioni hii kwenye uwanja wa Taifa, mpaka sasa ni kipindi cha pili na timu ziko sare kwa magoli 1-1 ambapo timu ya Mafunzo ilijipatia goli lake kupitia mchezaji Ali Othman Mpemba katika dakika ya 35 kipindi cha kwanza huku lile la Yanga likifungwa na Said Bahanuzi katika dakika ya 46 kipindi cha pili.

MAFUNZO: Hajji, Amour, Shaaban, Salum Said Shebe, Mmanga, Juma Othman Mmanga, ‘Selembe’,Juma Jaku, Abdulrahim, Ibrahim na Juma Hassan.

UPDATE:Toka Uwanja wa Taifa
Dakika 22' Hamisi Kiiza alishacheka na nyavu lakini anaambiwa alikuwa ameotea

Dakika ya 30, Young Africans 0 - 0 Mafunzo FC

Dakika ya 34, Ally Othman Mbanga anaipatia Mafunzo bao la kwanza

HALF TIME: YANGA 0-1 MAFUNZO

Dakika ya 46, Said Bahanunzi anaipatia Young Africans bao la kusawazisha. Young Africans 1 - 1 Mafunzo FC

Dakika ya 51, Young Africans inafanya mabadiliko, anaingia Jeryson Tegete anatoka Rashid Gumbo

Dakika 60: Yanga wamekuja na kasi kipindi cha pili, safu yake ya ushambuliaji inaonekana kuwa na uchu wa mabao

Dakikaya 64, Young Africans inafanya mabadiliko, anaingia Idrisa Rashid anatoka Stephano Mwasika

Dakika 69: Limepigwa shuti kali na limepanguliwa kwa ustadi na kipa wa Yanga Berko na kubaki majeruhi

Dakika 70: Shuti limemuacha Yew Berko akiwa majeruhi na sasa anaingia Ally Mustafa Barthez

Dakika ya 75, Young Africans 1 - 1 Mafunzo FC

Hamis Kiiiza anakosa bao la wazi dakika ya 77

Ball possesion Mafunzo 54 Yanga 46

Dakika 83: Yanga 1-1 Mafunzo

Dakika 83: Mafunzo: Anatoka Salum Shebe anaingia Kheir Salum Kheir

Dakika ya 86,mpira umesimama kwa muda mchezaji wa Mafunzo amepoteza fahamu

Ali Othman Mmanga wa Mafunzo ametolewa nje kwenye machela baada ya kujeruhiwa

Dakika 90: Zimeongezwa dakika 5 za nyongeza


Mafunzo wamecheza dakika 6 za mwishoni wakiwa pungufu baada ya kuwa wamemaliza sub zao zote

Mpira umemalizika, Young Africans 1 - 1 Mafunzo FC

Mshindi sasa kuamuliwa kwa matuta
PENATI:
Goal: Bahanuzi anafunga penati ya kwanza 1-0

Salum Said Shebe anafunga kwa upande wa mafunzo 1-1

Nadir Haroub Cannavaro anafunga kwa upande wa Yanga 2-1

Said Mussa Shaaban anakosa kwa upande wa mafunzo. Yanga wanaongoza 2-1

Hamis Kiiza anafunga kwa upande wa Yanga na sasa wanaongoza 3-1

Mafunzo wanafunga penati yao ya nne na sasa ni 3-2


Haruna Niyonzima anafunga kwa upande wa Yanga. 4-2

Juma Jaku anafunga kwa upande wa mafunzo 4-3

Athuman Idd Chuji anaipeleka Yanga nusu fainali baada ya kufunga penati ya mwisho kwa upande wa Yanga

Young Africans imeingia nusu fainali, baada ya kufunga penati 5-3 Wafunagji: Bahanunzi, Cannavaro, Kiiza, Niyonzima na Chuji

author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

4 comments

Hongera YANGA kwa kuifunga MAFUNZO

Reply

Tunawasubiria nyie ndala tuwafundishe ball kesho sie tunaisambaratisha Azam warudi Chamazii haraka....Yanga tunakuja SIMBA ngriiiiiiiiiiiiiiiii

Reply

Nani alifunga penalti ya tatu ya Mafunzo? Hamjasema

Reply

Juma Jaku anafunga anafunga kwa upande wa Mafunzo 4-3
Tunashukuru kwa kufuatilia kwa karibu Rundugai Blog

Reply

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top