1.Hali ya maji bwawa la Mtera inatishia shughuli ya uzalishaji wa umeme wa bwawa hilo na kidatu ambayo yanayochangia 280MW ktk gridi ya taifa.
2.Idara ya uhamiaji mkoani Pwani, imewakamata wachina 10 wafanyakazi wa kampuni ya Tansino 7 kati yao wakiwa hawana vibali vya kuishi nchini.
3.Kamati ya ulinzi na usalama mkoani Arusha imelitaka jeshi la polisi kuwasaidia waendesha Bodaboda kuzijua sheria za usalama barabarani.
4.Mamlaka ya elimu nchini (TEA) imezindua kampeni ya kuchangia ujenzi wa mabweni ya wasichana na kupata jumla ya milioni 37
5.Shirika la utetezi wa uhai wa binadamu na chama cha uimarishaji wa familia TZ limewataka wanawake watumie njia za asili za uzazi wa mpango.
6.Wakazi wa Mabibo stendi jijini Dar–es–salaam ,wako hatarini kupata kipindupindu na malaria kutokana na hali ya uchafu ya eneo hilo.
KWA HISANI YA ITV TANZANIA
KWA HISANI YA ITV TANZANIA
Post a Comment