Wanafunzi wa shule ya msingi Kawe B wakiwa darasani. Picha na HakiElimu
Mwalimu akiwa darasani kuitikia amri ya mahakama iliyowataka kurudi na kufundisha. Picha na HakiElimu
Wakati walimu wakiwa wanasubiri tamko la Chama Cha Walimu Tanzania kuhusu kukatisha mgomo, baadhi ya walimu wamerejea kazini siku ya leo na kuendelea kufundisha , HakiElimu imegundua. Mahudhurio katika baadhi ya shule zilizofikiwa na wadau wetu yalikuwa kama ifuatavyo:
- Shule ya Msingi Kawe B; walimu 17 kati ya 21
- Shule ya Msingi Ukwamani; walimu 15 kati ya 17
- Shule ya Msingi Makumbusho; walimu 25 kati ya 32
Walimu hao wamerejea huku wakiwa na manung'uniko na masikitiko juu ya uamuzi wa mahakama wa kukatisha mgomo. Hata hivyo, Shule zitafungwa siku ya leo mpaka tarehe 10 Septemba kupisha zoezi la sensa.
Via Haki Elimu
https://www.facebook.com/notes/hakielimu/baadhi-ya-walimu-warejea-kazini/424628280912978
This post was written by: Author Name
Your description comes here!
Get Free Email Updates to your Inbox!
Filed Under:
Jamii
on Friday, August 3, 2012
Post a Comment