............................................
Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Bububu unaotarajiwa kufanyika tarehe 16 septemba 2012 umeanza kuchukua kasi baada ya Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi Hussein Makungu kukabidhiwa fomu na msimamizi wa wa Uchaguzi mdogo jimbo la Bububu.
Ratiba ya Uchaguzi huo mdogo Jimbo la Bububu inaonyesha tarehe 30 agosti 2012 ndio siku ya Uteuzi wa wagombea na kuanzia tarehe 31 Agosti -15 Septemba 2012 ndio kipindi cha Kampeni na tarehe 16 Septemba 2012 ndio siku ya kupiga kura.
Katika Uchaguzi huo Mdogo Jimbo la Bububu Chama Cha Demokrasia na Maendeleo kimeamua kujitoa kushiriki katika uchaguzi huo.
Uchaguzi huo unafanyika kufuatia kifo cha mwakilishi wa zamani Salum Amour Mtondoo,kilichotokea Februari 14,mwaka huu.
Kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar vyama vilivyojitokeza kusimamisha wagombea ni CCM,CUF,TADEA,SAU,NCCR-MAGEUZI,Jahazi Asilia,AFP na NRA
|
Post a Comment